12-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Anachosema Anaporudi Kutoka Safari na Kuona Mji Wake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب مَا يقول إِذَا رجع وإذا رأى بلدته
12-Mlango Wa Anachosema Anaporudi Kutoka Safari na Kuona Mji Wake
وعن أنس رضي اللهُ عنه ، قَالَ : أقْبَلْنَا مَعَ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم حَتَّى إِذَا كُنَّا بِظَهْرِ الْمَدِينَةِ ، قَالَ : (( آيِبُونَ ، تَائِبُونَ ، عَابِدُونَ ، لِرَبِّنَا حَامِدُونَ )) فَلَمْ يَزَلْ يَقُولُ ذَلِكَ حَتَّى قَدِمْنَا المَدِينَةَ . رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa: Tulikuwa tunarudi pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mpaka tukafika mahali ambapo Madiynah ilikuwa inaonekana, hapo alisema: "Sisi ni wenye kurejea wenye kutubia wenye kumwabudu Rabb wetu wenye kumsifu." Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliendelea kukariri hayo mpaka tukawasili Madiynah. [Muslim]