14-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharamishwa Mwanamke Kusafiri Peke Yake
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب تحريم سفر المرأة وحدها
14-Mlango Wa Kuharamishwa Mwanamke Kusafiri Peke Yake
Hadiyth – 1
عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه، قَالَ: قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: (( لاَ يَحِلُّ لامْرَأَةٍ تُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَومِ الآخِرِ تُسَافِرُ مَسِيرَةَ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ إِلاَّ مَعَ ذِي مَحْرَمٍ عَلَيْهَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na Siku ya Mwisho kusafiri mwendo wa mchana kutwa na usiku kucha ila awe pamoja na mahramu yake." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 2
وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّهُ سَمِعَ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( لاَ يَخْلُوَنَّ رَجُلٌ بِامْرَأَةٍ إِلاَّ وَمَعَهَا ذُو مَحْرَمٍ ، وَلاَ تُسَافِرُ المَرْأةُ إِلاَّ مَعَ ذِي مَحْرَمٍ )) فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ : يَا رسولَ الله ، إنَّ امْرَأتِي خَرَجَتْ حَاجَّةً ، وَإنِّي اكْتُتِبْتُ في غَزْوَةِ كَذَا وَكَذَا ؟ قَالَ : (( انْطَلِقْ فَحُجَّ مَعَ امْرَأَتِكَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba amemsikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Mwanamme asikae faragha na mwanamke peke yao isipokuwa kuwe pamoja naye maharimu wake wala asisafiri mwanamke ila pamoja na maharimu wake. Yule mtu akamwambia: "Ee Rasuli wa Allaah! Hakika mke wangu ameazimia kuhiji nami nimejiandikisha kushiriki katika vita kadhaa na kadhaa?" Akasema: "Nenda kahiji na mkeo." [Al-Bukhaariy na Muslim]