01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora wa Kusoma Qur-aan
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل قراءة القرآن
01-Mlango Wa Ubora wa Kusoma Qur-aan
Hadiyth – 1
عن أَبي أُمَامَةَ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( اقْرَؤُوا القُرْآنَ ؛ فَإنَّهُ يَأتِي يَوْمَ القِيَامَةِ شَفِيعاً لأَصْحَابِهِ )) رواه مسلم .
Abu Umamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) Amesema kwamba amemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Isomeni Qur-aan kwani hakika itakuja Siku ya Qiyaamah kumuombea sahibu yake (aliyeisoma)." [Muslim]
Hadiyth – 2
وعن النَّوَّاسِ بنِ سَمْعَانَ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يقولُ : (( يُؤْتَى يَوْمَ القِيَامَةِ بِالقُرْآنِ وَأهْلِهِ الذينَ كَانُوا يَعْمَلُونَ بِهِ في الدُّنْيَا تَقْدُمُه سورَةُ البَقَرَةِ وَآلِ عِمْرَانَ ، تُحَاجَّانِ عَنْ صَاحِبِهِمَا )) رواه مسلم .
An-Nawwaas bin Sam'aan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Siku ya Qiyaamah italetwa Qur-aan pamoja na wale waliokuwa wakiitumia duniani. Itamtangulia Suratul Baqarah na Aal 'Imraan zikimtetea sahibu yake (wale waliokuwa wakizisoma katika maisha yao)." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن عثمان بن عفان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( خَيْرُكُمْ مَنْ تَعَلَّمَ الْقُرْآنَ وَعَلَّمَهُ )) رواه البخاري .
Imepokewa kutoka kwa 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mbora wenu ni yule aliyejifunza Qur-aan na akaifundisha." [Al-Bukhaariy]
Hadiyth – 4
وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( الَّذِي يَقْرَأُ القُرْآنَ وَهُوَ مَاهِرٌ بِهِ مَعَ السَّفَرَةِ الكِرَامِ البَرَرَةِ ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ لَهُ أجْرَانِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Yule ambaye anasoma Qur-aan naye ni mahiri katika hilo, atakuwa pamoja na Malaaikah na Mitume watukufu wenye kutii na yule ambaye anasoma Qur-aan na huku anaona ugumu na anapata shida, atapata malipo mawili." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na Ibn Maajah]
Hadiyth – 5
وعن أَبي موسى الأشعري رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي يَقْرَأُ القُرْآنَ مَثَلُ الأُتْرُجَّةِ : رِيحُهَا طَيِّبٌ وَطَعْمُهَا طَيِّبٌ ، وَمَثَلُ الْمُؤْمِنِ الَّذِي لاَ يَقْرَأُ القُرْآنَ كَمَثَلِ التَّمْرَةِ : لاَ رِيحَ لَهَا وَطَعْمُهَا حُلْوٌ ، وَمَثلُ المُنَافِقِ الَّذِي يقرأ القرآنَ كَمَثلِ الرَّيحانَةِ : ريحُهَا طَيِّبٌ وَطَعْمُهَا مُرٌّ ، وَمَثَلُ المُنَافِقِ الَّذِي لاَ يَقْرَأُ القُرْآنَ كَمَثلِ الحَنْظَلَةِ : لَيْسَ لَهَا رِيحٌ وَطَعْمُهَا مُرٌّ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mfano wa Muumini ambaye anasoma Qur-aan ni kama mfano wa mbalungi, harufu yake ni nzuri na ladha yake ni nzuri, na mfano wa Muumini ambaye hasomi Qur-aan mfano wake ni kama tende, haina harufu na ladha ni tamu. Na mfano wa mnafiki ambaye anasoma Qur-aan ni kama mfano wa mrehani, harufu yake ni nzuri na ladha yake ni chungu; na mfano wa mnafiki ambaye hasomi Qur-aan ni kama mfano wa handhala, hauna harufu na ladha yake ni chungu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawud, at-Tirmidhiy na An-Nasaai]
Hadiyth – 6
وعن عمر بن الخطاب رضي اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ اللهَ يَرْفَعُ بِهَذَا الكِتَابِ أقْوَاماً وَيَضَعُ بِهِ آخرِينَ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Umar bin Al-Khatwaab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah atawanyanyua watu kwa Kitabu hichi na kuwatwaza kwacho wengine." [Muslim]
Hadiyth – 7
وعن ابن عمر رضي اللهُ عنهما ، عن النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لاَ حَسَدَ إِلاَّ في اثْنَتَيْنِ : رَجُلٌ آتَاهُ اللهُ القُرْآنَ ، فَهُوَ يَقُومُ بِهِ آنَاء اللَّيْلِ وَآنَاءَ النَّهَارِ ، وَرَجُلٌ آتَاهُ اللهُ مَالاً ، فَهُوَ يُنْفِقُهُ آنَاءَ اللَّيْلِ وَآنَاءَ النَّهَارِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna husudu isipokuwa katika mambo mawili: Mtu amepewa na Allaah Qur-aan, akawa anaisoma nyakati za usiku na nyakati za mchana; na mtu amepewa mali na Allaah, naye anaitoa wakati wa usiku na wakati wa mchana." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 8
وعن البراءِ بن عازِبٍ رضي اللهُ عنهما ، قَالَ : كَانَ رَجُلٌ يَقْرَأُ سُورَةَ الْكَهْفِ ، وَعِنْدَهُ فَرَسٌ مَرْبُوطٌ بِشَطَنَيْنِ ، فَتَغَشَّتْهُ سَحَابَةٌ فَجَعَلَتْ تَدْنُو ، وَجَعَلَ فَرَسُه يَنْفِرُ مِنْهَا ، فَلَمَّا أصْبَحَ أتَى النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم فَذَكَرَ ذَلِكَ لَهُ ، فَقَالَ : (( تِلْكَ السَّكِينَةُ تَنَزَّلَتْ لِلقُرْآنِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Mtu mmoja alikuwa anasoma Suwrah Al-kahf, na mbele yake kuna farasi amefungwa kwa kamba mbili, ukungu ukamfunika yeye (wingu) na farasi wake akawa anaogopa huku anaruka ruka na kuukimbia. Kulipopambazuka alikwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumweleza kisa hicho. Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Hiyo ni As-Sakiynah (utulivu) unaoteremka kwa ajili ya Qur-aan." [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]
Hadiyth – 9
وعن ابن مسعودٍ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ قَرَأ حَرْفاً مِنْ كِتَابِ اللهِ فَلَهُ حَسَنَةٌ ، وَالحَسَنَةُ بِعَشْرِ أمْثَالِهَا ، لاَ أقول : ألم حَرفٌ ، وَلكِنْ : ألِفٌ حَرْفٌ ، وَلاَمٌ حَرْفٌ ، وَمِيمٌ حَرْفٌ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Na imepokewa kutoka kwa Ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye kusoma herufi moja kutoka kwa katika Kitabu cha Allaah atapata ujira mmoja, na ujira huu ni sawa na kumi mfano wake. Wala sisemi kuwa Alif Lam Miim ni herufi moja lakini Alif ni herufi na Lam ni herufi na Miim ni herufi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 10
وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ الَّذِي لَيْسَ في جَوْفِهِ شَيْءٌ مِنَ القُرْآنِ كَالبَيْتِ الخَرِبِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika yule ambaye kwamba hana moyoni mwake (yaani hakuhifadhi) chochote kaika Qur-aan ni kama nyumba iliyohamwa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
Hadiyth – 11
وعن عبد اللهِ بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( يُقَالُ لِصَاحِبِ الْقُرْآنِ : اقْرَأْ وَارْتَقِ وَرَتِّلْ كَمَا كُنْتَ تُرَتِّلُ في الدُّنْيَا ، فَإنَّ مَنْزِلَتَكَ عِنْدَ آخِرِ آية تَقْرَؤُهَا )) رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin 'Amru bin Al-'Aasw (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ataambiwa Mwenye (msomi) Qur-aan Siku ya Qiyaamah: "Soma Qur-aan, Upande daraja, Soma kama ulivyokuwa ukisoma duniani, kwani daraja yako iko mwisho wa ayah utakayosoma." [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]