11-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Ubora Wa kungojea Swalaah

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل انتظار الصلاة

11-Mlango Wa Ubora Wa kungojea Swalaah

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

وعن أبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لا يَزَالُ أحَدُكُمْ في صَلاَةٍ مَا دَامَتِ الصَّلاَةُ تَحْبِسُهُ ، لا يَمنَعُهُ أنْ يَنقَلِبَ إلى أهلِهِ إلاَّ الصَّلاةُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hatoacha mmoja wenu kuwa anahesabiwa yuko katika Swalaah madamu Swalaah ndiyo inayomzuia, hakuna kinachomzuia kurudi kwa familia yake isipokuwa Swalaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الْمَلائِكَةُ تُصَلِّي عَلَى أَحَدِكُمْ مَا دَامَ فِي مُصَلاَّهُ الَّذِي صَلَّى فِيهِ، مَا لَمْ يُحْدِثْ، تَقُولُ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لَهُ ، اللَّهُمَّ ارْحَمْهُ )) رواه البُخَارِيُّ .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Malaaikah wanamuombea msamaha na rehema mmoja wenu madamu amebaki kwenye msala alioswalia juu yake muda wa kuwa hajahuduthi hapo (hajatokwa na wudhuu), wakisema: "Ee Mola wetu msamehe, ee Mola wetu mrehemu." [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أنس رضي اللهُ عنه : أنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم أَخَّرَ لَيْلَةً صَلاَةَ العِشَاءِ إِلَى شَطْرِ اللَّيْلِ ثُمَّ أقْبَلَ عَلَيْنَا بِوَجْهِهِ بَعْدَمَا صَلَّى ، فَقَالَ : (( صَلَّى النَّاسُ وَرَقَدُوا ، وَلَمْ تَزَالُوا في صَلاَةٍ مُنْذُ انْتَظَرْتُمُوهَا )) رواه البُخَارِيُّ .

Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) anasimulia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliakhirisha usiku mmoja Swalaah ya Isha mpaka nusu ya usiku. Baada ya Swalaah alitukabili na kusema: "Baadhi ya watu waliswali na kwenda kulala lakini waliosubiri (ili kupata Swalaah ya jamaa) walikuwa katika Swalaah kuanzia walipoanza kuingojea." [Al-Bukhaariy]

 

 

Share