007-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Damu Ya Mnyama Aliyechinjwa
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
007- Vilivyoharamishwa Na Kitabu Cha Allaah:
Damu Ya Mnyama Aliyechinjwa (02)
2- Damu Ya Mnyama Aliyechinjwa
Si halali kula au kunywa damu ya mnyama aliyechinjwa. Ni kwa Neno Lake Ta’aalaa:
"حُرِّمَتْ عَلَيْكُمُ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ"
“Mmeharamishiwa nyamafu, na damu”. [Al-Maaidah: 03].
Ama damu kidogo kama ile inayobaki ndani ya mishipa ya mnyama aliyechinjwa ambayo ni vigumu kuepukana nayo, damu hii inasamehewa.
· Damu Iliyo Nje Ya Duara La Uharamu
Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
" أُحِلَّتْ لَنَا مَيْتَتَانِ وَدَمَانِ: ...... وَأَمَّا الدَّمَانِ: فالْكَبِدُ وَالطِّحَالُ "
“Tumehalalishiwa maiti mbili na damu mbili… na ama damu mbili, basi ni ini na wengu. [Hadiyth Swahiyh. Imepita nyuma kidogo].