23-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Sunnah Kabla na Baada ya Swalaah ya Ishaa
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب سنة العشاء بعدها وقبلها
23-Mlango Wa Sunnah Kabla na Baada ya Swalaah ya Ishaa
Hadiyth – 1
وعن ابن عمر رَضِيَ اللهُ عَنهُما ، قَالَ : صَلَّيْتُ مَعَ رَسُولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، رَكْعَتَيْنِ قَبْلَ الظُّهْرِ، وَرَكْعَتْينِ بَعْدَهَا، وَرَكْعَتَيْنِ بَعْدَ الجُمُعَةِ ، وَرَكْعَتَينِ بَعدَ المَغْرِبِ ، وَرَكْعَتَينِ بَعدَ العِشَاءِ . متفقٌ عَلَيهِ
Na Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Niliswali pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Rak'ah mbili kabla ya Adhuhuri, na Rak'ah mbili baada yake, Rak'ah mbili baada ya Ijumaa, na Rak'ah mbili baada ya Maghrib na Rak'ah mbili baada ya Isha." [Al-Bukhaariy na Muslim].
Hadiyth – 2
وعن عبد الله بن مُغَفَّلٍ رَضِيَ اللهُ عَنهُ ، قَالَ : قال رَسُول اللهِ صلى الله عليه وسلم : (( بَيْنَ كُلِّ أذَانَيْنِ صَلاَةٌ ، بَيْنَ كُلِّ أذَانَيْنِ صَلاَةٌ ، بَيْنَ كل أذانين صلاة )) قال في الثَّالِثةِ : (( لِمَنْ شَاءَ )) متفقٌ عَلَيهِ .
Imepokewa kutoka kwa 'Abdillaah bin Mughaffal kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Baina ya kila adhana mbili kuna Swalaah (makusudio ya adhana mbili ni baina ya adhana na iqamah), baina ya kila adhana mbili kuna Swalaah, baina ya kila adhana mbili kuna Swalaah." Akasema katika mara ya tatu: "Kwa mwenye kupenda." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai].