28-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kufaa Swalaah ya Dhuwhaa Kuanzia Linaponyanyuka Jua Mpaka Kupinduka (Zawaal), na Bora ni Kuiswali Wakati Jua Linapokuwa Kali

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تجويز صلاة الضحى من ارتفاع

الشمس إِلَى زوالها والأفضل أن تُصلَّى عِنْدَ

اشتداد الحر وارتفاع الضحى

28-Mlango Wa Kufaa Swalaah ya Dhuwhaa Kuanzia Linaponyanyuka Jua Mpaka Kupinduka (Zawaal), na Bora ni Kuiswali Wakati Jua Linapokuwa Kali

 

Alhidaaya.com

 

عن زيد بن أَرْقَم رضي اللهُ عنه : أنَّهُ رَأَى قَوْماً يُصَلُّونَ مِنَ الضُّحَى ، فَقَالَ : أمَا لَقَدْ عَلِمُوا أنَّ الصَّلاَةَ في غَيْرِ هذِهِ السَّاعَةِ أفْضَلُ ، إنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( صَلاَةُ الأَوَّابِينَ حِيْنَ تَرْمَضُ الفِصَالُ )) رواه مسلم .

Zayd bin Arqam (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Aliona watu wanaswali Dhuwhaa, akasema: Ama kwa hakika hawajajua kwamba Swalaah katika wakati mwingine usiokuwa huu ni bora zaidi kwani Rasuli wa Allaah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Swalaah ya Awwaabiyn (wanaorudi kutoka kwa kughafika wakaja kuhudhuria na kutoka katika dhambi kuelekea kwa tauba na msamaha) ni wakati wa jua kali ambapo watoto wa ngamia hukusanywa." [Muslim]

 

 

 

Share