36-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kupiga Mswaki na Mambo ya Kimaumbile

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب فضل السواك وخصال الفطرة

36-Mlango Wa Fadhila za Kupiga Mswaki na Mambo ya Kimaumbile

 

Alhidaaya.com

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( لَوْلاَ أنْ أشُقَّ عَلَى أُمَّتِي - أَوْ عَلَى النَّاسِ - لأَمَرْتُهُمْ بِالسِّوَاكِ مَعَ كُلِّ صَلاَةٍ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kama sikuhofia kwa Ummah wangu - au watu - ningewaamuru wapige mswaki kabla ya kila Swalaah." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]

 

Hadiyth – 2

وعن حُذَيْفَةَ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم إِذَا قَامَ مِن النَّومِ يَشُوصُ فَاهُ بِالسِّوَاكِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Hudhayfah (Radhwiya Allaahu 'anhu) : Alipokuwa akiamka usingizini usiku,  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisafisha kinywa chake kwa mswaki." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd na An-Nasaai]

 

Hadiyth – 3

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : كُنَّا نُعِدُّ لِرسولِ الله صلى الله عليه وسلم سِوَاكَهُ وَطَهُورَهُ ، فَيَبْعَثُهُ اللهُ مَا شَاءَ أنْ يَبْعَثَهُ مِنَ اللَّيْلِ ، فَيَتَسَوَّكُ ، وَيَتَوضَّأُ وَيُصَلِّي . رواه مسلم .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Tulikuwa tukimtayarisha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mswaki wake na maji yake ya wudhuu, na alikuwa akianza kupiga mswaki na kisha kutawadha na kuswali pindi atakapoamshwa na Allaah usiku." [Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أنس رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أكْثَرْتُ عَلَيْكُمْ في السِّوَاكِ )) رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Ninawahimizeni sana nyinyi muwe mkitumia mswaki." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 5

وعن شريح بن هانىءٍ ، قَالَ : قلت لعائشة رضي اللهُ عنها : بأَيِّ شَيْءٍ كَانَ يَبْدَأُ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم إِذَا دَخَلَ بَيْتَهُ ؟ قالت : بِالسِّوَاكِ . رواه مسلم .

Amesema Shurayh bin Haani': Nilimuuliza 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) : "Ni kitu gani alikuwa anaanza nacho Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapoingia nyumbani kwake?" Akajibu: "Alikuwa akipiga mswaki." [Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي موسى الأشعري رضي اللهُ عنه ، قَالَ : دَخلتُ عَلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم وَطَرَفُ السِّوَاكِ عَلَى لِسَانِهِ . متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ مسلمٍ .

Amesema Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) : Niliingia kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ncha ya mswaki ipo mdomoni mwake." [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Muslim]

 

Hadiyth – 7

وعن عائشة رضي الله عنها : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( السِّوَاكُ مَطْهَرَةٌ لِلْفَمِ مَرْضَاةٌ للرَّبِّ )) رواه النسائي وابنُ خُزَيْمَةَ في صحيحهِ بأسانيدَ صحيحةٍ .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mswaki unasafisha mdomo na unamridhisha Rabb." [An-Nasaai na Ibn Khuzaymah katika Swahiyh yake kwa Isnaad zilizo Swahiyh]

 

Hadiyth – 8

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( الفِطْرَةُ خَمْسٌ ، أَوْ خَمْسٌ مِنَ الفِطْرَةِ : الخِتَانُ ، وَالاسْتِحْدَادُ ، وَتَقْلِيمُ الأظْفَارِ ، وَنَتْفُ الإبطِ ، وَقَصُّ الشَّارِبِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Fitrah ni mambo matano au mambo matano ni katika Fitrah: Kutahiri, kunyoa nywele za kinena (sehemu za siri), kung'oa nywele za kwapani, kukata kucha na kupunguza sharubu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 9

وعن عائشة رضي الله عنها ، قالت : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( عَشْرٌ مِنَ الفِطْرَةِ : قَصُّ الشَّارِبِ ، وَإعْفَاءُ اللِّحْيَةِ ، وَالسِّوَاكُ ، وَاسْتِنْشَاقُ المَاءِ ، وَقَصُّ الأظْفَارِ ، وَغَسْلُ البَرَاجِمِ ، وَنَتف الإبْطِ ، وَحَلْقُ العَانَةِ ، وَانْتِقَاصُ المَاءِ )) قَالَ الرَّاوِي : وَنَسِيْتُ العَاشِرَةَ إِلاَّ أنْ تَكُونَ المَضمَضَةُ . قَالَ وَكِيعٌ - وَهُوَ أحَدُ رُواتِهِ - انْتِقَاصُ المَاءِ : يَعْنِي الاسْتِنْجَاءِ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mambo kumi ni katika Fitrah: Kupunguza sharubu, na kufuga ndevu bila ya kuzipunguza, na kupiga mswaki, na kusafisha pua kwa kupandisha maji puani, na kukata kucha, na kuosha mashina ya vidole, na kung'oa nywele za kwapani, na kunyoa nywele za kinena na kujisafisha kwa maji baada ya kwenda haja." Amesema mpokezi: "Na nimesahau jambo la kumi ila huenda ikawa ni kusukutuwa." Akasema Waki'un mmoja miongoni mwa wapokezi: "Intiqaaswul Maa'ina maana ya kujiosha baada ya haja (ndogo au kubwa)." [Muslim]

 

Hadiyth – 10

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أحْفُوا الشَّوَارِبَ وَأعْفُوا اللِّحَى )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Punguzeni sharubu na fugeni ndevu." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

 

Share