42-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kula Daku na Kuichelewesha Maadamu Hakutahofiwa Kuingia kwa Alfajiri
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب فضل السحور وتأخيره
مَا لَمْ يخش طلوع الفجر
42-Mlango Wa Fadhila za Kula Daku na Kuichelewesha Maadamu Hakutahofiwa Kuingia kwa Alfajiri
Hadiyth – 1
عن أنس رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( تَسَحَّرُوا ؛ فَإنَّ في السُّحُورِ بَرَكَةً )) متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kuleni daku kwani ndani ya daku mna baraka." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An- Nasaaiy]
Hadiyth – 2
وعن زيدِ بن ثابتٍ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : تَسَحَّرْنَا مَعَ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، ثُمَّ قُمْنَا إِلَى الصَّلاَةِ . قِيلَ : كَمْ كَانَ بينهما ؟ قَالَ : قَدْرُ خَمْسين آيةً . متفقٌ عَلَيْهِ .
Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Thaabit (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Tulikula daku pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Alllahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kisha tukasimama kuswali. Akauliza: "Ni muda gani kati ya kula na kuswali?" Akasema: "Kiasi cha ayah hamsini." [Al-Bukhaariy, Muslim na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 3
وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ لرسولِ الله صلى الله عليه وسلم مُؤَذِّنَانِ : بِلاَلٌ وَابْنُ أُمِّ مَكْتُومٍ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنْ بِلالاً يُؤَذِّنُ بِلَيْلٍ ، فَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يُؤَذِّنَ ابْنُ أُمِّ مَكْتُومٍ )) قَالَ : وَلَمْ يَكُنْ بَيْنَهُمَا إِلاَّ أنْ يَنْزِلَ هَذَا وَيَرْقَى هَذَا . متفقٌ عَلَيْهِ .
Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na waadhini wawili: Bilaal na Ibn Ummi Maktuwm. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Akasema: "Hakika Bilaal anaadhini usiku, kwa hivyo kuleni na kunyweni mpaka aadhini Ibn Ummi Maktuwm." Akasema: "Na hakukuwa na tofauti baina yao ila kushuka huyu na kupanda huyu mwingine." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 4
وعن عمرو بن العاص رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( فَصْلُ مَا بَيْنَ صِيَامِنَا وصِيَامِ أهْلِ الكِتَابِ ، أكْلَةُ السَّحَرِ )) رواه مسلم .
Imepokewa kutoka kwa 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaahu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Tofauti baina ya funga yetu na ya Ahluk Kitaab (Waliopewa Kitabu) ni kula daku." [Muslim]