51-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kupendeza Kufunga Siku Tatu Kila Mwezi
Riyaadhw Asw-Swaalihiyn
باب استحباب صوم ثلاثة أيام من كل شهر
51-Mlango Wa Kupendeza Kufunga Siku Tatu Kila Mwezi
Hadiyth – 1
وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، قَالَ : أوْصاني خَلِيلي صلى الله عليه وسلم بِثَلاثٍ : صِيَامِ ثَلاَثَةِ أيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ، وَرَكْعَتَي الضُّحَى ، وَأنْ أُوتِرَ قَبْلَ أنْ أنَامَ . متفقٌ عَلَيْهِ .
Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Kipenzi changu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameniusia vitu vitatu, nisiviache mpaka ninakufa: "Kufunga siku tatu kila mwezi, kuswali Swalaah ya Dhuwhaa na kulala baada ya kuswali Witri." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Hadiyth – 2
وعن أَبي الدرداءِ رضي اللهُ عنه ، قَالَ : أوصاني حَبِيبـي صلى الله عليه وسلم بِثَلاثٍ لَنْ أدَعَهُنَّ مَا عِشتُ : بِصِيَامِ ثَلاثَةِ أيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ، وَصَلاَةِ الضُّحَى ، وبِأنْ لاَ أنَامَ حَتَّى أُوتِرَ . رواه مسلم .
Amesema Abu Dardaa (Radhwiya Allaahu 'anhu): Amenisusia kipenzi changu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kushikamana na vitu vitatu nami sitaacha maadamu ni hai: "Kufunga siku tatu kila mwezi, na kuswali Swalaah ya Dhuwhaa na nisilale mpaka niswali Witri." [Muslim]
Hadiyth – 3
وعن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( صَوْمُ ثَلاَثَةِ أيَّامٍ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ صَوْمُ الدَّهْرِ كُلِّهِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .
'Abdillaah bin 'Amruw bin Al-'Aas (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kufunga siku tatu katika kila mwezi ni sawa na funga ya milele." [Al-Bukhaariy na Muslim]
Hadiyth – 4
وعن مُعاذة العدوية : أنها سألت عائشةَ رَضِيَ اللهُ عنها : أكَانَ رسول الله صلى الله عليه وسلم يَصُومُ مِنْ كُلِّ شَهْرٍ ثَلاَثة أيَّامٍ ؟ قالت : نَعَمْ . فقلتُ : مِنْ أيِّ الشَّهْرِ كَانَ يَصُومُ ؟ قالت : لَمْ يَكُنْ يُبَالِي مِنْ أيِّ الشَّهْرِ يَصُومُ . رواه مسلم .
Mu'aadhah Al-'Adawiyyah alimuuliza 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): "Je, Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anafunga siku tatu kila mwezi?" Akasema: "Ndio." Nikamuuliza: "Alikuwa akifunga katika mwezi gani?" Akasema: "Alikuwa hajali ni katika mwezi gani aliokuwa akifunga." [Muslim]
Hadiyth – 5
وعن أَبي ذر رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إِذَا صُمْتَ مِنَ الشَّهْرِ ثَلاَثاً، فَصُمْ ثَلاَثَ عَشْرَةَ، وَأرْبَعَ عَشْرَةَ ، وَخَمْسَ عَشْرَةَ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .
Kutoka kwa Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Unapofunga siku tatu katika kila mwezi basi funga tarehe kumi na tatu (13), na kumi na nne (14) na kumi na tano (15)." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]
Hadiyth – 6
وعن قتادة بن مِلْحَان رضي اللهُ عنه ، قَالَ : كَانَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم يَأمُرُنَا بِصِيَامِ أيَّامِ البِيضِ : ثَلاثَ عَشْرَةَ ، وَأرْبَعَ عَشْرَةَ ، وَخَمْسَ عَشْرَةَ . رواه أَبُو داود .
Qataadah bin Milhaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anatuamuru tufunge siku Nyeupe: Tarehe kumi na tatu (13), na kumi na nne (14) na kumi na tano (15)." [Abu Daawuwd]
Hadiyth – 7
وعن ابن عباس رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَ رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم لاَ يُفْطِرُ أيَّامَ البِيضِ في حَضَرٍ وَلاَ سَفَرٍ . رواه النسائي بإسنادٍ حسن .
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alikuwa hali katika siku Nyeupe akiwa mjini wala safarini." [An-Nasaaiy kwa Isnaad iliyo Hasan]