01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Wajibu wa Hijjah na Fadhila Zake

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب وجوب الحج وفضله

01-Mlango Wa Wajibu wa Hijjah na Fadhila Zake

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾ 

Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah Ni Mkwasi kwa walimwengu. [Aal-'Imraan: 97]

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( بُنِي الإسْلاَمُ عَلَى خَمْسٍ : شَهَادَةِ أنْ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ ، وَأنَّ مُحَمَّداً رسولُ اللهِ ، وَإقَامِ الصَّلاَةِ ، وَإيتَاءِ الزَّكَاةِ ، وَحَجِّ البَيْتِ ، وَصَوْمِ رَمَضَانَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwake Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Umejengwa Uislamu juu ya nguzo tano: Kukiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kuhiji na kufunga mwezi wa Ramadhwaan." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : خَطَبَنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : (( أيُّهَا النَّاسُ ، قَدْ فَرَضَ اللهُ عَلَيْكُم الحَجَّ فَحُجُّوا )) فَقَالَ رَجُلٌ : أكُلَّ عَامٍ يَا رَسولَ اللهِ ؟ فَسَكَتَ ، حَتَّى قَالَهَا ثَلاثاً . فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( لَوْ قُلْتُ نَعَمْ لَوَجَبَتْ ، وَلَمَا اسْتَطَعْتُمْ )) ثُمَّ قَالَ : (( ذَرُوني مَا تَرَكْتُكُمْ ؛ فَإنَّمَا هَلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ بِكَثْرَةِ سُؤالِهِمْ ، وَاخْتِلاَفِهِمْ عَلَى أنْبِيَائِهِمْ ، فَإذَا أمَرْتُكُمْ بِشَيءٍ فَأتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ ، وَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَن شَيْءٍ فَدَعُوهُ )) رواه مسلم .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Alituhutubia akasema: "Enyi watu! Hakika Allaah amewafaradhia Hijjah, hivyo Hijini." Mtu mmoja akauliza: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, ni kila mwaka?" Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alinyamaza mpaka yule mtu akauliza swali hilo mara tatu. Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Lau nilisema ndiyo, ingewalazimu kuhiji kila mwaka na hamngeweza." Kisha akasema: "Kwa hivyo acheni kuniuliza niliyoyaacha, kwani waliangamia waliokuwa kabla yenu kwa wingi wa maswali yao na kukhitalifiana kwa Manabiy wao. Ninapowaamrisha jambo yafanyeni kiasi mnachoweza na nikiwakataza kitu basi kiacheni." [Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سُئِلَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم أيُّ العَمَلِ أفْضَلُ ؟ قَالَ : (( إيمَانٌ بِاللهِ وَرسولِهِ )) قيل : ثُمَّ ماذا ؟ قَالَ : (( الجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ )) قِيلَ : ثُمَّ مَاذَا ؟ قَالَ : (( حَجٌّ مَبرُورٌ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Aliulizwa: "Ni amali gani iliyo bora?" Akasema: "Kumuamini Allaah na Rasuli Wake." Pakasemwa: "Kisha ni ipi?" Akasema: "Kupoigana jihadi katika njia ya Allaah." Akaulizwa tena: "Kisha ni ipi?" Akasema: "Hijaah iliyokubalika, (Mabruwr)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم ، يقول : (( مَنْ حَجَّ ، فَلَمْ يَرْفُثْ ، وَلَمْ يَفْسُقْ ، رَجَعَ كَيَوْمِ وَلَدَتْهُ أمُّهُ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Abu uraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu a'layhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Atakayehiji bila ya kufanya madhambi na bila ya kuruka mipaka ya kisheria atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake  (bila ya kuwa na dhambi)." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik na At-Tirmidhiy]

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول اللهِ صلى الله عليه وسلم ، قال : (( العُمْرَةُ إِلَى

 

العُمْرَةِ كَفَّارَةٌ لِمَا بَينَهُمَا ، وَالحَجُّ المَبْرُورُ لَيْسَ لَهُ جَزَاءٌ إِلاَّ الجَنَّةَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kutoka Umrah moja hadi Umrah nyingine ni kafara ya kilicho kati yake na Hajj Mabruwr haina malipo isipokuwa Pepo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 6

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها ، قَالَت : قُلْتُ : يَا رسول الله ، نَرَى الجِهَادَ أفْضَلَ العَمَلِ ، أفَلاَ

 

نُجَاهِدُ ؟ فَقَالَ : (( لَكُنَّ أفْضَلُ الجِهَادِ : حَجٌّ مَبْرُورٌ )) رواه البخاري .

Amesema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa): Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Tunaona kuwa Jihaad ndiyo amali bora kabisa. Je tupigane?" Akasema: "Kwenu nyinyi wanawake Jihaadi bora ni Hajj Mabruwr." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 7

وعن عائشة رَضِيَ اللهُ عنها : أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( مَا مِنْ يَوْمٍ

 

أكْثَرَ مِنْ أن يَعْتِقَ اللهُ فِيهِ عَبْداً مِنَ النَّارِ مِنْ يَوْمِ عَرَفَةَ )) رواه مسلم .

Na imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hapana siku yoyote ambayo Allaah Huacha waja wengi zaidi huru na Moto kuliko siku ya 'Arafah." [Muslim]

 

Hadiyth – 8

وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( عُمْرَةٌ في

 

رَمَضَانَ تَعْدِلُ حَجَّةً – أَوْ حَجَّةً مَعِي )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Umrah inayofanywa katika mwezi wa Ramadhwaan ni sawa (kwa thawabu) na Hijjah au Hijjah pamoja nami." [Al-Bukhaariy na muslim]

 

Hadiyth – 9

وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ امرأة قالت : يَا رسول الله ، إنَّ فَرِيضَةَ اللهِ عَلَى

 

عِبَادِهِ في الحَجِّ ، أدْرَكَتْ أَبي شَيْخاً كَبِيراً ، لاَ يَثْبُتُ عَلَى الرَّاحِلَةِ أفَأحُجُّ عَنْهُ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ

 

)) متفقٌ عَلَيْهِ .

Na imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa mwanamke mmoja alisema: "Ee Rasuli wa Allaah! Faradhi ya Allaah juu ya waja wake katika Hijjah imemfikia baba yangu akiwa mzee mno, naye hawezi kukaa juu ya mnyama, je nimuhijie?" Akamjibu: "Ndiyo." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 10

وعن لقيط بن عامر رضي الله عنه : أنَّه أتى النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : إنَّ أَبِي

 

شَيْخٌ كَبِيرٌ ، لاَ يَسْتَطِيعُ الحَجَّ ، وَلاَ العُمْرَةَ ، وَلاَ الظَّعَنَ ؟ قَالَ : (( حُجَّ عَنْ أبِيكَ وَاعْتَمِرْ ))

 

رواه أَبُو داود والترمذي ، وقال : (( حديث حسن صحيح )) .

Imepokewa kutoka kwa Laqiitw bin 'Aamir (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuuliza: "Hakika baba yangu ni mkongwe, hivyo hawezi kusafiri wala kupanda kipando kwa ajili ya kutekeleza Hijjah wala kufanya Umrah?" [Abu Daawuwd na At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Hadiyth – 11

وعن السائب بن يزيد رضي الله عنه ، قَالَ : حُجَّ بي مَعَ رسولِ اللهِ صلى الله عليه وسلم ،

 

في حَجةِ الوَدَاعِ ، وَأنَا ابنُ سَبعِ سِنينَ . رواه البخاري .

Amesema As-Saaib bin Yaziyd (Radhwiya Allaahu 'anhu): Nilihiji pamoja na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijjatul Wadaa' (Hijjah ya kuaga) na wakati huo nilikuwa mtoto wa miaka saba." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 12

وعن ابن عباس رضي الله عنهما : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم لَقِيَ رَكْباً بالرَّوْحَاءِ ،

 

فَقَالَ : (( مَنِ القَوْمُ ؟ )) قالوا: المسلِمُونَ . قالوا : مَنْ أنْتَ ؟ قَالَ : (( رسولُ اللهِ )) .

 

فَرَفَعَتِ امْرَأةٌ صَبيّاً ، فَقَالَتْ : ألِهَذَا حَجٌّ ؟ قَالَ : (( نَعَمْ ، وَلَكِ أجْرٌ )) رواه مسلم .

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikutana na msafara katika Rawhaa (ni kitongoji karibu na mji wa Madiynah) akawauliza: "Hawa ni watu gani?" Wakasema: "Waislamu." Wakasema: "Nani wewe?", Akassema: "Rasuli wa Allaah." Mwanamke mmoja akamuinua mtoto mdogo, akauliza: "Je, huyu ana Hijja?" Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Ndiyo, nawe una ujira (kwa hilo)." [Muslim]

 

Hadiyth – 13

عن أنسٍ رضي الله عنه: أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم حَجَّ عَلَى رَحْلٍ وَكانت

 

زَامِلَتهُ . رواه البخاري .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alihiji akiwa amepanda kipando (ngamia) ambaye pia alibeba chakula na vitu vyengine vinavyohitajika (yaani hakuna mnyama wa kumbeba yeye (Nabiy) na mwingine wa kubeba mzigo mwingine). [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 14

وعن ابن عباسٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : كَانَتْ عُكَاظُ ، وَمَجِنَّةُ ، وَذُو المَجَازِ أسْوَاقاً في

 

الجَاهِلِيَّةِ ، فَتَأثَّمُوا أن يَتَّجِرُوا في المَوَاسِمِ ، فَنَزَلَتْ : [ لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَنْ تَبْتَغُوا فَضْلاً

 

مِنْ رَبِّكُمْ ] [ البقرة : 198 ] في مَوَاسِمِ الحَجِّ . رواه البخاري .

Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: 'Ukaadh na Majinnah na Dhul Majaaz yalikuwa masoko katika kipindi cha Ujahiliyyah (ujinga kabla kipindi cha kutumilizwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Baada ya kuja Uislamu baadhi ya watu walidhania kuwa ni makosa na madhambi kufanya biashara katika makosa haya wakati wa Hijjah. Hapo Allaah Aliteremsha Ayah ifuatayo: "Hapana dhambi kwenu kutafuta Fadhila toka kwa Rabb wenu." [Al-Baqarah: 198] [Al-Bukhaariy]

 

 

 

 

 

 

 

Share