04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kumfanyia Hisani Mtumwa

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل الإحسان إِلَى المملوك

04-Mlango Wa Fadhila za Kumfanyia Hisani Mtumwa

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَاعْبُدُوا اللَّـهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَىٰ وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا ﴿٣٦﴾

Na mwabuduni Allaah na wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni ihsaan wazazi wawili na jamaa wa karibu, na mayatima, na masikini na jirani mwenye ujamaa na jirani asiye na ujamaa na rafiki wa karibu, na msafiri aliyeishiwa masurufu, na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Hakika Allaah Hapendi mwenye majivuno mwenye kujifakharisha. [An-Nisaa: 36]

 

Hadiyth – 1

وعنِ المَعْرُورِ بن سُوَيْدٍ ، قَالَ : رَأيْتُ أَبَا ذَرٍ رضي اللهُ عنه ، وَعَلَيهِ حُلَّةٌ وَعَلَى غُلاَمِهِ مِثْلُهَا، فَسَأَلْتُهُ عَنْ ذَلِكَ، فَذَكَرَ أنَّهُ قَدْ سَابَّ رَجُلاً عَلَى عَهْدِ رسول الله صلى الله عليه وسلم، فَعَيَّرَهُ بِأُمِّهِ ، فَقَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( إنَّكَ امْرُؤٌ فِيكَ جَاهِليَّةٌ هُمْ إخْوَانُكُمْ وَخَوَلُكُمْ جَعَلَهُمُ الله تَحْتَ أيديكُمْ ، فَمَنْ كَانَ أَخُوهُ تَحْتَ يَدِهِ ، فَلْيُطْعِمْهُ مِمَّا يَأكُلُ ، وَلْيُلْبِسْهُ مِمَّا يَلْبَسُ ، وَلاَ تُكَلِّفُوهُمْ مَا يَغْلِبُهُمْ ، فَإنْ كَلَّفْتُمُوهُمْ فَأَعِينُوهُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Al-Ma'ruwr bin Suwayd amesema: Nilimuona Abu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) akiwa amevaa mavazi sawa na mtumwa wake, hivyo nikamuuliza kuhusu hilo. Akanieleza kuwa wakati wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mtu mmoja alimtukana mtu mwingine naye akamjibu kwa kumtukania mamake. Hapo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia: "Hakika wewe una chembe ya tabia za kijahiliya. Hakika hao ni ndugu zenu na watumishi wenu Allaah amewaweka mikononi mwenu, basi yule ambae ndugu yake yuko mikononi mwake amlishe anachokula yeye na amvishe anachovaa yeye na wala msiwalazimishe kinachowashinda mkiwalazimisha basi wasaidieni." [Al-Bukhaariy, Muslim na Abu Daawuwd]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( إِذَا أَتَى أحَدَكُمْ خَادِمُهُ بِطَعَامِهِ ، فَإنْ لَمْ يُجْلِسْهُ مَعَهُ ، فَلْيُنَاوِلْهُ لُقْمَةً أَوْ لُقْمَتَيْنِ أَوْ أُكْلَةً أَوْ أُكْلَتَيْنِ ؛ فَإنَّهُ وَلِيَ عِلاَجَهُ )) رواه البخاري .

Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapoletwa mmoja wenu chakula na mtumishi wake, na ikiwa hatamwambia akae ale pamoja naye basi ampatie tonge moja au mawili kwani yeye amefanya juhudi katika kukitayarisha." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share