04-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Karama za Mawalii na Fadhila Zao

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب كرامات الأولياء وفضلهم

04-Mlango Wa Karama za Mawalii na Fadhila Zao

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللَّـهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ﴿٦٢﴾

Tanabahi! Hakika Vipenzi wa Allaah hawana khofu na wala hawatohuzunika.

الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ﴿٦٣﴾

Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.

لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ لِكَلِمَاتِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ﴿٦٤﴾

Watapata bishara katika uhai wa dunia na katika Aakhirah. Hakuna mabadiliko katika Maneno ya Allaah. Huko ndiko kufuzu adhimu. [Yuwnus: 62-64]

وَهُزِّي إِلَيْكِ بِجِذْعِ النَّخْلَةِ تُسَاقِطْ عَلَيْكِ رُطَبًا جَنِيًّا ﴿٢٥﴾

Na tingisha kuelekea kwako shina la mtende, litakuangushia tende safi zilizoiva na zilizo tayari kuchumwa. 

فَكُلِي وَاشْرَبِي وَقَرِّي عَيْنًا ۖ  ﴿٢٦﴾

Basi kula na kunywa. [Maryam: 25-26]

كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾ 

Kila Zakariyyaa alipoingia kwake katika chumba cha kuswalia alikuta kwake vyakula. Akasema: Ee Maryam! Umepata wapi hivi? Akasema: Hivi ni kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu. [Aal-'Imraan: 37]

وَإِذِ اعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّـهَ فَأْوُوا إِلَى الْكَهْفِ يَنشُرْ لَكُمْ رَبُّكُم مِّن رَّحْمَتِهِ وَيُهَيِّئْ لَكُم مِّنْ أَمْرِكُم مِّرْفَقًا ﴿١٦﴾

Na mkijitenga nao na vile wanavyoviabudu badala ya Allaah, basi kimbilieni pangoni. Rabb wenu Atakufungulieni Rahmah Zake, na Atakutengenezeeni wepesi katika mambo yenu.

وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَت تَّزَاوَرُ عَن كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَت تَّقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ  ﴿١٧﴾

Na (ungeliwaona basi ungelikuwa) unaliona jua linapochomoza linaelemea pango lao kwa upande wa kulia, na linapokuchwa linawakwepa upande wa kushoto [Al-Kahf: 16-17]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي محمد عبد الرحمان بن أَبي بكرٍ الصديق رضي الله عنهما : أنَّ أَصْحَابَ الصُّفّةِ كَانُوا أُنَاساً فُقَرَاءَ وَأَنَّ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ مَرَّةً : (( مَنْ كَانَ عِنْدَهُ طَعَامُ اثْنَيْنِ ، فَلْيَذْهَبْ بثَالِثٍ ، وَمنْ كَانَ عِنْدَهُ طَعَامُ أرْبَعَةٍ ، فَلْيَذْهَبْ بِخَامِسٍ بِسَادِسٍ )) أَوْ كما قَالَ ، وأنَّ أَبَا بكرٍ رضي اللهُ عنه ، جَاءَ بِثَلاَثَةٍ ، وانْطَلَقَ النبيّ صلى الله عليه وسلم بعَشَرَةٍ ، وأنَّ أَبَا بَكرٍ تَعَشَّى عِنْدَ النبيّ صلى الله عليه وسلم ، ثُمَّ لَبِثَ حَتَّى صَلَّى العِشَاءَ ، ثُمَّ رَجَعَ ، فجاءَ بَعْدَ مَا مَضَى مِنَ اللَّيْلِ مَا شَاءَ اللهُ . قالت امْرَأتُهُ : مَا حَبَسَكَ عَنْ أضْيَافِكَ ؟ قَالَ : أوَما عَشَّيْتِهمْ ؟ قالت: أَبَوْا حَتَّى تَجِيءَ وَقَدْ عَرَضُوا عَلَيْهِمْ ، قَالَ : فَذَهَبتُ أَنَا فَاخْتَبَأْتُ ، فَقالَ : يَا غُنْثَرُ ، فَجَدَّعَ وَسَبَّ ، وقالَ : كُلُوا لاَ هَنِيئاً وَاللهِ لا أَطْعَمُهُ أَبَداً ، قَالَ : وايْمُ اللهِ مَا كُنَّا نَأخُذُ مِنْ لُقْمَةٍ إلا ربا من أسفلِها أكثرَ منها حتى شبعوا ، وصارتْ أكثرَ مما كانتْ قبلَ ذلكَ ، فنظرَ إليها أبو بكر فقالَ لامرأتِهِ : يا أختَ بني فراسٍ ما هذا ؟ قالت : لا وقُرَّةِ عيني لهي الآنَ أكثرُ منها قبلَ ذلكَ بثلاثِ مراتٍ ! فأكل منها أبو بكرٍ وقال : إنَّما كانَ ذلكَ من الشيطانِ ، يعني : يمينَهُ . ثم أكلَ منها لقمةً ، ثُمَّ حَمَلَهَا إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَصْبَحَتْ عِنْدَهُ. وَكَانَ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمٍ عَهْدٌ، فَمَضَى الأجَلُ ، فَتَفَرَّقْنَا اثْنَيْ عَشَرَ رَجُلاً ، مَعَ كُلِّ رَجُلٍ مِنْهُمْ أُنَاسٌ ، اللهُ أعْلَمُ كَمْ مَعَ كُلِّ رَجُلٍ فَأَكَلُوا مِنْهَا أَجْمَعُونَ .

وَفِي رِوَايةٍ : فَحَلَفَ أَبُو بَكْرٍ لا يَطْعَمُهُ ، فَحَلَفَت المَرْأَةُ لا تَطْعَمُهُ ، فَحَلَفَ الضَّيْفُ . - أَو الأَضْيَافُ - أنْ لاَ يَطْعَمُهُ أَوْ يَطْعَمُوهُ حَتَّى يَطْعَمَهُ . فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ : هذِهِ مِنَ الشَّيْطَانِ ! فَدَعَا بالطَّعَامِ فَأكَلَ وأكَلُوا ، فَجَعَلُوا لا يَرْفَعُونَ لُقْمَةً إِلاَّ رَبَتْ مِنْ أسْفَلِهَا أَكْثَرُ مِنْهَا ، فَقَالَ : يَا أُخْتَ بَني فِرَاسٍ ، مَا هَذَا ؟ فَقَالَتْ : وَقُرْةِ عَيْنِي إنَّهَا الآنَ لأَكْثَرُ مِنْهَا قَبْلَ أنْ نَأكُلَ ، فَأكَلُوا ، وَبَعَثَ بِهَا إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَذَكَرَ أنَّهُ أكَلَ مِنْهَا .

وَفِي رِوايَةٍ : إنَّ أَبَا بكْرٍ قَالَ لِعَبْدِ الرَّحْمانِ : دُونَكَ أضْيَافَكَ ، فَإنِّي مُنْطلقٌ إِلَى النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، فَافْرُغْ مِنْ قِراهُم قَبْلَ أنْ أَجِيءَ ، فَانْطَلَقَ عَبْدُ الرَّحْمانِ ، فَأَتَاهُمْ بما عِنْدَهُ ، فَقَالَ : اطْعَمُوا ؛ فقالوا : أين رَبُّ مَنْزِلِنا ؟ قَالَ : اطْعَمُوا ، قالوا : مَا نحنُ بِاكِلِينَ حَتَّى يَجِيءَ رَبُّ مَنْزِلِنَا ، قَالَ : اقْبَلُوا عَنْا قِرَاكُمْ ، فَإنَّهُ إنْ جَاءَ وَلَمْ تَطْعَمُوا ، لَنَلْقَيَنَّ مِنْهُ فأبَوْا ، فَعَرَفْتُ أنَّهُ يَجِدُ عَلَيَّ ، فَلَمَّا جَاءَ تَنَحَّيْتُ عَنْهُ ، فَقَالَ : مَا صَنَعْتُمْ ؟ فَأخْبَرُوهُ ، فَقَالَ : يَا عَبْدَ الرَّحمانِ ، فَسَكَتُّ : ثُمَّ قَالَ : يَا عَبْدَ الرَّحْمانِ ، فَسَكَتُّ ، فَقَالَ: يَا غُنْثَرُ أقْسَمْتُ عَلَيْكَ إنْ كُنْتَ تَسْمَعُ صَوتِي لَمَا جِئْتَ ! فَخَرَجْتُ ، فَقُلْتُ : سَلْ أضْيَافَكَ ، فقالُوا : صَدَقَ ، أتَانَا بِهِ ، فَقَالَ : إنَّمَا انْتَظَرْتُمُونِي والله لا أَطْعَمُهُ اللَّيْلَةَ . فَقَالَ الآخَرُونَ : واللهِ لا نَطْعَمُهُ حَتَّى تَطْعَمَهُ فَقَالَ : وَيْلَكُمْ مَا لَكُمْ لا تَقْبَلُونَ عَنَّا قِرَاكُمْ ؟ هَاتِ طَعَامَكَ ، فَجَاءَ بِهِ ، فَوَضَعَ يَدَهُ فَقَالَ : بِسْمِ اللهِ ، الأولَى مِنَ الشَّيْطَانِ ، فَأَكَلَ وَأَكَلُوا . متفق عَلَيْهِ

Kutoka kwa Abu Muhammad Abdur-Rahmaan bin Abu Bakar As-Swiddiq (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa watu wa Suffah walikuwa ni watu mafakiri na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mwenye chakula cha kuwatosha watu wawili aende naye watatu (katika hao watu wa Suffah), na kama cha wanne aende naye wa tano au sita." Au kama alivyosema. Na Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alichukua watu watatu na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaondoka na watu kumi. Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikula chakula cha jioni kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kisha akabaki hadi iliposwaliwa Ishaa, kisha akarudi akabaki na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akaja nyumbani baada ya kupita usiku muda alioutaka Allaah. Mkewe akamuuliza: "Nini kilicho kuchelewesha ukawaacha wageni wako?" Akamjibu: "Kwani hukuwapa chakula cha jioni?" Mkewe akajibu: "Wamepewa wakakataa kula mpaka ufike." Abdur-Rahmaan akasema: "Mimi nikaenda kujificha, (kwa kumuogopa Abu Bakar) wakati huo huo akaniita, akasema: 'We mpumbavu!' na akanitukana na akaniambia, 'Kula, hufai kukaribishwa. Wa-Allaahi! Sili kabisa kwa yamini ya Allaah." Hatukuwa tunachukuwa tonge isipokuwa kilicho kuwa chini yake kilizidi zaidi ya kilichokuwepo. Tulikula hadi tukashiba, lakini chakula kikawa kimebaki kuliko vile kilivyokuwa kabla ya kuliwa. Abu Bakar akakiangalia akakikuta kama kilivyo kuwa au zaidi. Akamuuliza mkewe: "Ee dada wa Bani Firas! Nini hiki?" Mkewe akajibu: "Sielewi, naapa kwa tulizo la jicho langu! Hivi sasa ni kinga zaidi ya kilivyo kuwa kwa mara tatu." Abu Bakr akala, kisha akasema: "Hakika si vingine bali ile ilikuwa kutokana na shetani, akikusudia ile yamini yake." Kisha akala katika chakula hicho tonge moja kisha akakipeleka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), kikaamkia kwake. Kulikuwa na mkataba kati yetu na watu fulani, muda ukapita Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatugawa katika makundi ya watu kumi na wawili, kila kimoja kikaongozwa na mtu mmoja. Allaah Ndiye Anayejua ni wangapi katika watu hao walioongoza na kiongozi mmoja? Wakala chakula hicho wote."

Na katika riwaayah nyengine: "Abu Bakar aliapa kuwa hatakula, na mkewe pia naye akaapa kuwa hatakula na akaapa mgeni au wageni kuwa naye hatakua au hawatakula mpaka ale (Abu Bakar). Akasema Abu Bakar: 'Hii ni kutokana na shetani.' Akaitisha chakula, akala na wote wakala. Hatukuwa tunachukuwa tonge isipokuwa kilicho kuwa chini yake kilizidi zaidi ya (kilichokuwepo). Akamuuliza mkewe: 'Ee dada wa Bani Firas! Nini hiki?' Mkewe akajibu: 'Naapa kwa tulizo la jicho langu! Hivi sasa ni kinga zaidi ya kilivyo kuwa kabla hatujala.' Wakala na akakipeleka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). ambaye alieleza kuwa alikula kutoka kwa hicho chakula." 

Na katika riwaayah nyingine: Hakika Abu Bakar alimwambia Abdur-Rahman: "Washughulikie wageni wako kwani mimi ninakwenda kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na uwalishe vyema kabla sijarudi." Hivyo Abdur-Rahmaan aliondoka na kuwaletea chakula walichokuwa nacho na kuwaambia: :kuleni." Wakasema: "Yu wapi mwenye nyumba?" Akawaambia: "Kuleni." Wakasema: "Sisi hatuli mpaka afike mwenye nyumba." Akawaambia: "Tafadhali kubalini ukarimu wetu na mule (chakula), kwani atakaporudi na kukuta hamjakula atakasirika sana." Lakini wageni walikataa katakata. Nikajua kuwa atakaporudi atakasirika akiona wageni hawajakula. Aliporudi nilijificha (ili asinipate), naye akasema: "Je, mumewafanyia nini wageni?" Wakampasha habari ya yaliotokea (yaani wageni kukataa kula), na hapo akaita: "Ee Abdur-Rahmaan." Nami nikanyamaza kimya. Kisha akaita tena: "Ee Abdur-Rahmaan", nami nikakaa kimya. Hapo akasema: "Ee mpumbavu! Ninaapa kuwa lau wanisikia basi utakuja hapa." Hapo nikatoka na kumwambia: "Waulize wageni wako." Nao wakasema: "Anasema kweli, kwani alikuja na chakula." Hapo Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akasema: "Hakika nyinyi mumeningojea mimi bila ya udhuru wowote, Wa-Allaahi sitakula chakula usiku wa leo."  Wakasema wengine: "Wa-Allaahi! Nasi hatutakula mpaka nawe ule chakula hiki." Akasema: "Ole wenu! Muna nini mbona munakataa ukarimu wetu? Leteni chakula." Kikaletwa chakula, naye (Abu Bakr) akaingiza mkono wake na kusema: "BismiLLaahi! Kiapo changu kilikuwa ni kutokana na shetani." Hivyo, yeye na kutokana na wageni wake wakala chakula hicho." [Al-Bukhaariy, Muslim na Ahmad]   

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لَقَدْ كَانَ فيما قَبْلَكُمْ مِنَ الأُمَمِ نَاسٌ مُحَدَّثُونَ، فَإنْ يَكُ في أُمَّتِي أحدٌ فإنَّهُ عُمَرُ)) . رواه البخاري.

ورواه مسلم من رواية عائشة .

وفي روايتهما قَالَ ابن وهب : (( محَدَّثُونَ )) أيْ مُلْهَمُونَ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika kulikuwa katika waliokuwa kabla yenu watu Muhaddathuwn (wanasema maneno yanayowafikiana na haki). Hivyo, kukiwa katika ummah wangu yeyote mwenye sifa hiyo basi ni 'Umar." [Al-Bukhaariy, na imepokewa na muslim kutoka riwaayah ya 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa)].

 

Hadiyth – 3

وعن جابر بنِ سُمْرَةَ رضي الله عنهما ، قَالَ : شَكَا أهْلُ الكُوفَةِ سَعْداً يعني : ابنَ أَبي وقاص رضي اللهُ عنه ، إِلَى عمر بن الخطاب رضي اللهُ عنه فَعَزَلَهُ ، واسْتَعْمَلَ عَلَيْهِمْ عَمَّاراً ، فَشَكَوا حَتَّى ذَكَرُوا أنَّهُ لا يُحْسِنُ يُصَلِّي ، فَأَرْسَلَ إِلَيْهِ ، فَقَالَ : يَا أَبَا إسْحَاقَ ، إنَّ هَؤُلاَءِ يَزْعَمُونَ أنَّكَ لا تُحْسِنُ تُصَلِّي ، فَقَالَ : أَمَّا أنا واللهِ فَإنِّي كُنْتُ أُصَلِّي بِهِمْ صَلاَةَ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، لا أُخْرِمُ عَنْها ، أُصَلِّي صَلاَتَي العِشَاءِ فَأَرْكُدُ فِي الأُولَيَيْنِ ، وَأُخِفُّ في الأُخْرَيَيْنِ . قَالَ : ذَلِكَ الظَّنُّ بِكَ يَا أَبَا إسْحَاقَ ، وأَرْسَلَ مَعَهُ رَجُلاً - أَوْ رِجَالاً - إِلَى الكُوفَةِ يَسْأَلُ عَنْهُ أهْلَ الكُوفَةِ ، فَلَمْ يَدَعْ مَسْجِداً إِلاَّ سَأَلَ عَنْهُ ، وَيُثْنُونَ مَعْرُوفاً ، حَتَّى دَخَلَ مَسْجِداً لِبَنِي عَبْسٍ ، فَقَامَ رَجُلٌ مِنْهُمْ ، يُقالُ لَهُ أُسَامَةُ بْنُ قَتَادَةَ ، يُكَنَّى أَبَا سَعْدَةَ، فَقَالَ: أمَا إذْ نَشَدْتَنَا فَإنَّ سَعْداً كَانَ لا يَسِيرُ بالسَّرِيَّةِ وَلاَ يَقْسِمُ بالسَّوِيَّةِ ، وَلاَ يَعْدِلُ في القَضِيَّةِ . قَالَ سَعْدٌ : أمَا وَاللهِ لأَدْعُونَّ بِثَلاَثٍ : اللَّهُمَّ إنْ كَانَ عَبْدُكَ هَذَا كَاذِباً ، قَامَ رِيَاءً ، وَسُمْعَةً ، فَأَطِلْ عُمُرَهُ ، وَأَطِلْ فَقْرَهُ ، وَعَرِّضْهُ لِلْفِتَنِ . وَكَانَ بَعْدَ ذَلِكَ إِذَا سُئِلَ يَقُولُ : شَيْخٌ كَبيرٌ مَفْتُونٌ ، أَصَابَتْنِي دَعْوَةُ سَعْدٍ . قَالَ عَبدُ الملكِ بن عُمَيْرٍ الراوي عن جابرِ بنِ سَمُرَةَ : فَأنا رَأَيْتُهُ بَعْدُ قَدْ سَقَطَ حَاجِبَاهُ عَلَى عَيْنَيْهِ مِنَ الكِبَرِ ، وإنَّهُ لَيَتَعَرَّضُ لِلْجَوارِي فِي الطُّرُقِ فَيَغْمِزُهُنَّ . متفق عَلَيْهِ .

Amesema Jaabir bin Samurah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Watu wa Kufah walimshitakia Sa'ad bin Abu Waqqaas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye alikuwa Iiwali wao kwa 'Umar bin Al-Khaattaab (Radhwiya Allaahu 'anhu). Akaondolewa na kuwekwa badala yake 'Ammaar (Radhwiya Allaahu 'anhu). Katika mashtaka yao walimshutuhumu kuwa Sa'ad haswalishi vizuri. 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu)alimuita Sa'ad aje Madiynah, (alipofika) alimuuliza: "Ee Abu Ishaaq! Watu wa Kufah wanakushtaki kuwa wewe hujui kuswalisha vizuri." Akajibu: "Ama mimi Wa-Allaahi, nilikuwa nawaswalisha Swalaah ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) bila kubadilisha hata kidogo. Nilikuwa nawaswalisha Swalaah ya Ishaa, nikirefusha rakaa mbili za mwanzo na kuhafifisha rakaa mbili za mwisho." Akasema: "Hakika hiyo ndiyo iliyokuwa dhana yangu kwako, ee Abu Ishaaq." 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alimtuma mtu mmoja au wawili pamoja naye kuelekea Kufah ili kuchunguza kuhusu mashtaka hayo kutoka kwa watu wa Kufah. Wachunguzi hawa walipita katika kila Msikiti na kuwauliza watu kuhusu Sa'ad na watu wote walimsifu kwa wema wake mpaka wakafika katika Msikiti wa Bani 'Abs. Na hapo alisimama mtu mmoja miongoni mwao, ambaye anaitwa Usamah bin Qataadah, aliyekuwa na kunyah ya Abu Sa'dah, akasema: "Ama mkiwa mnataka kauli yetu, basi jueni kuwa Sa'ad hashiriki katika Jihadi, wala hagawi ngawira sawasawa, wala hahukumu kwa uadilifu." Hapo akasema Sa'ad: "Ama Wa-Allaahi, nitakuombea juu ya mambo matatu: "Ee Rabb Wangu! Ikiwa mja Wako huyu ni muongo, amesimama kwa ajili ya kujionyesha na kupata umaarufu, Mrefushie umri wake, na Umzidishie ufukara wake na Mtie katika mitihani na fitna." Na alikuwa baada ya hapo akiulizwa kuhusu hali yake, husema: "Mzee mkongwe aliye fitinika, imenisibu mimi duaa ya Sa'ad." Amesema Abdul-Malik bin 'Umayr, mpokezi kutoka kwa Jaabir bin Samurah (Radhwiyah Allaahu 'anhu): "Hakika mimi nilimuona (huyu Usamah) baada ya nyusi zake kuanguka juu ya macho yake kwa sababu ya ukongwe. Na hakika yeye alikuwa akizurura barabarani huku akiwabembeleza na kuwatongoza wasichana." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 4

وعن عروة بن الزبير : أنَّ سعيد بن زيد بن عمرو بن نُفَيلٍ رضي اللهُ عنه ، خَاصَمَتْهُ أَرْوَى بِنْتُ أوْسٍ إِلَى مَرْوَانَ بْنِ الحَكَمِ ، وادَّعَتْ أنَّهُ أخَذَ شَيْئاً مِنْ أرْضِهَا ، فَقَالَ سعيدٌ : أنا كُنْتُ آخُذُ شَيئاً مِنْ أرْضِهَا بَعْدَ الَّذِي سَمِعْتُ مِنْ رسول الله صلى الله عليه وسلم !؟ قَالَ : مَاذَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ؟ قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يقول : (( مَنْ أخَذَ شِبْراً مِنَ الأرْضِ ظُلْماً ، طُوِّقَهُ إِلَى سَبْعِ أرْضِينَ )) فَقَالَ لَهُ مَرْوَانُ : لا أسْألُكَ بَيِّنَةً بَعْدَ هَذَا ، فَقَالَ سعيد : اللَّهُمَّ إنْ كَانَتْ كاذِبَةً ، فَأعْمِ بَصَرَها ، وَاقْتُلْهَا في أرْضِها ، قَالَ : فَما ماتَتْ حَتَّى ذَهَبَ بَصَرُهَا ، وَبَيْنَما هِيَ تَمْشِي في أرْضِهَا إذ وَقَعَتْ في حُفْرَةٍ فَماتَتْ . متفق عَلَيْهِ .

وفي روايةٍ لِمُسْلِمٍ عن محمد بن زيد بن عبد الله بن عُمَرَ بِمَعْنَاهُ ، وأنه رآها عَمْيَاءَ تَلْتَمِسُ الجُدُرَ تقولُ : أصابَتْنِي دَعْوَةُ سَعيدٍ ، وأنَّها مَرَّتْ عَلَى بِئرٍ في الدَّارِ الَّتي خَاصَمَتْهُ فِيهَا ، فَوَقَعَتْ فِيهَا ، وكانتْ قَبْرَها .

Imepokewa kutoka kwa 'Urwah bin az-Zubayr kuwa Sa'iyd bin Zayd bin 'Amruw bin Nufayl (Radhwiya Allaahu 'anhu) alishtakiwa na Arwaa bint Aws kwa Marwaan bin al-Hakam, na kudai kuwa Sa'iyd amechukua sehemu ya ardhi yake. Akasema: "Nawezaje mimi kuchukua kipande cha ardhi yake baada ya kumsikia Rasuli wa Allaah?" Akamuuliza Marwaan: "Umemsikia nini Rasuli wa Allaah?" Akasema: "Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: 'Mwenye kuchukua shibiri moja ya ardhi kwa dhulma, atafanywa avae mkufu wa ardhi saba." Akamwambia yeye Marwaan: "Sitokuomba ushahidi mwingine wowote baada ya huu." Sa'iyd akasema: "Ee Rabb Wangu! Ikiwa yeye (aliye leta madai) ni muongo basi mfanye kipofu na muue katika ardhi yake." Akasema: "Hakuaga dunia mpaka baada ya kuwa kipofu na alipokuwa anatembea katika ardhi yake alianguka kwenye shimo na kufariki." [Al-Bukhaariy na Muslim]

Na katika riwaayah ya Muslim kutoka kwa Muhammad bin Zayd bin 'Abdillaah bin 'Umar kwa maana yake kuwa alimuona huyu mwanamke akiwa kipofu akishika shika kuta huku akisema: "Imenipata mimi duaa ya Sa'iyd." Na wakati mmoja alipita kwenye kisima cha nyumba aliyozozana kwayo, akaanguka ndani yake na hilo ndilo likawa kaburi lake."

 

Hadiyth – 5

وعن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما ، قَالَ : لَمَّا حَضَرَتْ أُحُدٌ دعَانِي أَبي من اللَّيلِ فَقَالَ : مَا أُرَاني إِلاَّ مَقْتُولاً في أوْلِ مَنْ يُقْتَلُ من أصْحَابِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، وإنِّي لا أَتْرُكُ بَعْدِي أَعَزَّ عَلَيَّ مِنْكَ غَيْرَ نَفْسِ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، وإنَّ عَلَيَّ دَيْناً فَاقْضِ ، وَاسْتَوْصِ بِأَخَوَاتِكَ خَيْراً ، فَأصْبَحْنَا ، فَكَانَ أَوَّلَ قَتِيلٍ ، وَدَفَنْتُ مَعَهُ آخَرَ في قَبْرِهِ ، ثُمَّ لَمْ تَطِبْ نَفْسِي أنْ أتْرُكَهُ مَعَ آخَرَ ، فَاسْتَخْرَجْتُهُ بَعْدَ سِتَّةِ أشْهُرٍ ، فإذا هُوَ كَيَوْمِ وَضَعْتُهُ غَيْرَ أُذنِهِ ، فَجَعَلْتُهُ في قَبْرٍ عَلَى حِدَةٍ . رواه البخاري .

Amesema Jaabir bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Baba yangu aliniita usiku kabla ya Vita vya Uhud, akaniambia: "Naona mimi nitakuwa wa kwanza miongoni mwa Swahaaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuuliwa kesho. Na hakika, mimi sijaacha kipenzi kwangu baada ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ila wewe. Na hakika mimi nina deni, hivyo lilipe na ninakuusia uwatendee wema dada zako." Kulipopambazuka (na vita kuanza, hakika akawa wa kwanza kufa shahidi na nikamzika pamoja na wengine katika kaburi moja. Kisha nafsi yangu haikupendelea kumuacha yeye (babangu) pamoja na wengine katika kaburi moja, hivyo nikamfukua baada ya miezi sita na kuukuta mwili wake katika hali ile ile aliyozikiwa nayo isipokuwa kovu (alama) iliyokuwa kwenye sikio lake. Nikauzika mwili wake katika kaburi jengine." [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 6

وعن أنس رضي اللهُ عنه : أنَّ رجلين مِنْ أصحاب النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، خَرَجَا مِنْ عِنْدِ النَّبيِّ صلى الله عليه وسلم ، في لَيْلَةٍ مُظْلِمَةٍ وَمَعَهُمَا مِثْلُ المِصْبَاحَيْنِ بَيْنَ أَيْديهِمَا . فَلَمَّا افْتَرَقَا ، صَارَ مَعَ كُلِّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا وَاحِدٌ حَتَّى أتَى أهْلَهُ .

رواهُ البُخاري مِنْ طُرُقٍ ؛ وفي بَعْضِهَا أنَّ الرَّجُلَيْنِ أُسَيْدُ بنُ حُضير ، وَعَبّادُ بنُ بِشْرٍ رضي الله عنهما .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa watu wawili miongoni mwa Swahaaba wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walitoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) usiku mmoja wa giza totoro na wakawa pamoja nao mfano wa taa mbili katika mikono yao. Lakini pindi walipoachana kila mmoja wao akawa na taa yake mpaka walipofika nyumbani kwao." [Al-Bukhaariy kwa njia tofauti]

Na katika mapokezi mengine ya Al-Bukhaariy amesema kwamba watu wawili hao ni Usayd Ibn Hudhwaiyr na Ubbada Ibn Bishri (Radhwiya Allaahu 'anhumaa)

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه قَالَ : بعث رسول الله صلى الله عليه وسلم عَشْرَة رَهْطٍ عَيْناً سَرِيَّة، وأمَّرَ عَلَيْهَا عاصِمَ بنَ ثَابِتٍ الأنْصَارِيَّ رضي اللهُ عنه ، فانْطلقوا حَتَّى إِذَا كَانُوا بالهَدْأةِ ؛ بَيْنَ عُسْفَانَ وَمَكَّةَ ؛ ذُكِرُوا لِحَيٍّ مِنْ هُذَيْل يُقالُ لَهُمْ : بَنُو لحيانَ ، فَنَفَرُوا لَهُمْ بِقَريبٍ مِنْ مِئَةِ رَجُلٍ رَامٍ ، فَاقْتَصُّوا آثَارَهُمْ ، فَلَمَّا أحَسَّ بِهِمْ عَاصِمٌ وأصْحَابُهُ ، لَجَأُوا إِلَى مَوْضِعٍ ، فَأَحاطَ بِهِمُ القَوْمُ ، فَقَالُوا : انْزِلُوا فَأَعْطُوا بِأيْدِيكُمْ وَلَكُمُ العَهْدُ وَالمِيثَاقُ أنْ لا نَقْتُلَ مِنْكُمْ أحَداً . فَقَالَ عَاصِمُ بنُ ثَابِتٍ : أَيُّهَا القَوْمُ ، أَمَّا أنا ، فَلاَ أنْزِلُ عَلَى ذِمَّةِ كَافِرٍ : اللَّهُمَّ أَخْبِرْ عَنَّا نَبِيَّكَ صلى الله عليه وسلم ، فَرَمُوهُمْ بِالنّبْلِ فَقَتلُوا عَاصِماً ، وَنَزَلَ إلَيْهِمْ ثَلاَثَةُ نَفَرٍ عَلَى العَهْدِ والمِيثاقِ، مِنْهُمْ خُبَيْبٌ، وَزَيدُ بنُ الدَّثِنَةِ وَرَجُلٌ آخَرُ. فَلَمَّا اسْتَمْكَنُوا مِنْهُمْ أطْلَقُوا أوْتَارَ قِسِيِّهِمْ ، فَرَبطُوهُمْ بِهَا . قَالَ الرَّجُلُ الثَّالِثُ : هَذَا أوَّلُ الغَدْرِ واللهِ لا أصْحَبُكُمْ إنَّ لِي بِهؤُلاءِ أُسْوَةً ، يُريدُ القَتْلَى ، فَجَرُّوهُ وعَالَجُوهُ ، فأبى أنْ يَصْحَبَهُمْ ، فَقَتَلُوهُ ، وانْطَلَقُوا بِخُبَيبٍ ، وزَيْدِ بنِ الدَّثِنَةِ ، حَتَّى بَاعُوهُما بِمَكَّةَ بَعْدَ وَقْعَةِ بَدْرٍ ؛ فابْتَاعَ بَنُو الحارِثِ بن عامِرِ بنِ نَوْفَلِ بنِ عبدِ مَنَافٍ خُبيباً ، وكان خُبَيْبٌ هُوَ قَتَلَ الحَارِثَ يَوْمَ بَدْرٍ . فَلِبثَ خُبَيْبٌ عِنْدَهُمْ أسيراً حَتَّى أجْمَعُوا عَلَى قَتْلِهِ ، فاسْتَعَارَ مِنْ بَعْضِ بَنَاتِ الحَارثِ مُوسَى يَسْتَحِدُّ بِهَا فَأعَارَتْهُ ، فَدَرَجَ بُنَيٌّ لَهَا وَهِيَ غَافِلَةٌ حَتَّى أَتَاهُ ، فَوَجَدتهُ مُجْلِسَهُ عَلَى فَخْذِهِ وَالموسَى بِيَدِهِ ، فَفَزِعَتْ فَزْعَةً عَرَفَهَا خُبَيْبٌ . فَقَالَ : أَتَخَشَيْنَ أن أقْتُلَهُ مَا كُنْتُ لأَفْعَلَ ذَلِكَ ! قالت : واللهِ مَا رَأيْتُ أسيراً خَيراً مِنْ خُبَيْبٍ ، فواللهِ لَقَدْ وَجَدْتُهُ يَوماً يَأكُلُ قِطْفاً مِنْ عِنَبٍ في يَدِهِ وإنَّهُ لَمُوثَقٌ بِالحَدِيدِ وَمَا بِمَكَّةَ مِنْ ثَمَرَةٍ ، وَكَانَتْ تَقُولُ : إنَّهُ لَرِزْقٌ رَزَقَهُ اللهُ خُبَيْباً . فَلَمَّا خَرَجُوا بِهِ مِنَ الحَرَمِ لِيَقْتُلُوهُ في الحِلِّ، قَالَ لَهُمْ خُبَيْبٌ : دَعُونِي أُصَلِّي رَكْعَتَيْنِ ، فَتَرَكُوهُ ، فَرَكَعَ رَكْعَتَيْنِ فَقَالَ : واللهِ لَوْلاَ أنْ تَحْسَبُوا أنَّ مَا بِي جَزَعٌ لَزِدْتُ : اللَّهُمَّ أحْصِهِمْ عَدَداً ، وَاقْتُلهُمْ بِدَدَاً ، وَلاَ تُبْقِ مِنْهُمْ أَحَداً . وقال :

فَلَسْتُ أُبَالِي حِيْنَ أُقْتَلُ مُسْلِماً
 

 

عَلَى أيِّ جَنْبٍ كَانَ للهِ مَصْرَعِي


وَذَلِكَ في ذَاتِ الإلَهِ وإنْ يَشَأْ


 

يُبَارِكْ عَلَى أوْصَالِ شِلْوٍ مُمَزَّعِ
 

 

وكان خُبَيبٌ هُوَ سَنَّ لِكُلِّ مُسْلِمٍ قُتِلَ صَبْراً الصَّلاَةَ . وأخْبَرَ - يعني : النبيّ صلى الله عليه وسلم - أصْحَابَهُ يَوْمَ أُصِيبُوا خَبَرَهُمْ ، وَبَعَثَ نَاسٌ مِنْ قُرَيْشٍ إِلَى عَاصِمِ بنِ ثَابتٍ حِيْنَ حُدِّثُوا أَنَّهُ قُتِلَ أن يُؤْتَوا بِشَيءٍ مِنْهُ يُعْرَفُ ، وكَانَ قَتَلَ رَجُلاً مِنْ عُظَمائِهِمْ ، فَبَعَثَ الله لِعَاصِمٍ مِثْلَ الظُّلَّةِ مِنَ الدَّبْرِ فَحَمَتْهُ مِنْ رُسُلِهِمْ ، فَلَمْ يَقْدِروا أنْ يَقْطَعُوا مِنْهُ شَيْئاً . رواه البخاري .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alituma Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kikosi cha watu kumi chini ya uamiri wa 'Aaswim bin Thaabit Al-Answaariyy (Radhwiya Allaahu 'anhu). wakaondoka kuelekea sehemu waliyotumwa mpaka wakafika sehemu inayoitwa Had'ah, baina ya 'Usfaan na Makkah, waliambiwa kuhusu wao ukoo wa Lahay unaotokana na Hudhayl, wanaoitwa Banu Lahyaan. Wakawafuata wapiga mishale na mikuki wanaokaribia mia moja, wakazifuata nyayo zao. 'Aaswin na Swahaaba wenziwe walipohisi kuwa wanafuatwa walipanda kwenye mlima na kujificha hapo na wale maadui wakawazunguka. Wakawaambia: "Shukeni chini, tunaahidi kuwa iwapo mtakuja kwetu hatutamwua katika nyinyi mtu yeyote." Akasema 'Aaswim bin Thaabit: "Enyi kaumi! Ama mimi, sitashuka chini kuwa chini ya dhima na ahadi ya kafiri. Ee Rabb Wangu! Mpashe habari Nabiy Wako (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu hali yetu." Wakaanza kuwarushia mishale, hivyo kumuua 'Aaswim na wakateremka kwao watatu kwa ahadi na mkataba waliopewa, akiwemo Khubayb, na Zayd bin ad-Dathinah na mtu mwengine (wengine sita walikuwa wameuliwa pamoja na Amiri wao, 'Aaswim). Walipoteremka wakawafanyia khiana na kuwafunga kwa kamba za pinde zao, yule mtu wa tatu akasema: "Huu ni mwanzo wa khiana. Wa-Allaahi, sitafuatana nanyi na nitafuata kigezo cha wenzangu waliotangulia, akimaanisha wale waliouliwa." Wakamkokota na wakamshawishi afuatane nao, lakini alikataa katakata kufanya hivyo, nao wakamwua na kisha kuondoka na Khubayb na Zayd bin ad-Dathinah. Wakawauza huko Makkah na walikuwa wamewaua baadhi ya viongozi wa Makkah katika Vita vya Badr. Banu Al-Haariyh bin 'Aamir bin Nawfal bin 'Abdi Manaaf walimnunua Khubayb, kwani Khubayb ndiye aliyemuua Haarith katika Vita vya Badr. Khubayb alikaa kwao hali ya kuwa ni mfungwa mpaka walipoamua kumuua. Siku moja Khubayb aliomba wembe kutoka kwa mmoja wa binti za Haarith ili kukata kucha zake. Wakati huo huo mtoto wa huyu mama aliondoka huku akiwa naye. Alipomkumbuka alikuja kumkuta kwenye mapaja ya khubayb, naye akiwa na wembe mkononi mwake. Mama huyu alibabaika sana mpaka akatambua hilo Khubayb, ambaye alimwambia: "Unahofia kuwa nitamuua? Siwezi kabisa kufanya kitendo hicho." Akasema: "Wa-Allaahi! Sijauona mfungwa bora kuliko Khubayb. Wa-Allaahi, nilimuona siku moja akila kikonyo cha zabibu na hali mikono yake imefungwa na minyororo na katika mji wa Makkah hakuna matunda hayo." Na alikuwa akisema (yaani huyu mwanamke): "Ni hakika kuwa hiyo ilikuwa ni riziki aliyoruzukiwa Khubayb na Allaah." Walipotoka naye nje ya mipaka ya Haram ili kwenda kumuua, Khubayb aliwaambia: "Niacheni niswali rakaa mbili." Wakamwacha, naye akaswali hizo rakaa mbili, kisha akasema: "Naapa kwa jina la Allaah, lau si kuwa - mutasema kuwa haya ninayofanya ni kulalamika ningeongezea (kuswali rakaa zingine)." Kisha akaomba duaa: "Ee Rabb Wangu wadhibiti kwa idadi wauwe mmoja mmoja na usimbakishe katika wao mtu yeyote." Kisha akasoma mashairi yake: Sijali ninapouliwa nikiwa Muislamu, Kwa ubavu gani nitaelekea kwa Allaah. Na hiki kifo changu ni kwa ajili ya Allaah, Na Yeye Atavibariki vipande vya mwili wangu vilivyo katwa. Na alikuwa Khubayb mtu wa kwanza aliyeleta Sunnah kwa kila Muislamu aliyeuliwa akiwa katika hali ya kusubiri ya kuswali rakaa mbili. Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalhi wa sallam) aliwapasha habari Swahaaba zake siku waliyouliwa. Na Maquraysh waliwatuma watu kwenda kuhakikisha kifo cha 'Aaswim bin Thaabit (Radhwiya Allaahu 'anhu) pindi walipopata habari ya kuuliwa kwake na waletewe chochote katika wanachokijua katika mwili wake ili apate kujulikana kuwa ndiye. Na 'Aaswim alikuwa amemwua mtu mkubwa miongoni mwa watukufu wao (wa Makkah). Allaah Akapeleka mfano wa kiwingu cha manyigu, yakamlinda na wajumbe hao hawakuweza kutaka chochote katika mwili wake. [Al-Bukhaariy]

 

Hadiyth – 8

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : مَا سَمِعْتُ عمر رضي اللهُ عنه يقولُ لِشَيءٍ قَطُّ : إنِّي لأَظُنُّهُ كَذَا ، إِلاَّ كَانَ كَمَا يَظُنُّ . رواه البخاري .

Amesema Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa): Sikumsikia 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akisema kwa ajili ya kitu chochote kamwe: Hakika mimi nadhania kuwa jambo hili ni hivi isipokuwa huwa kama alivyo dhania. [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share