001-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Taarifu Ya Viapo

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ

 

Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

01- Taarifu Ya Viapo

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

[Taarifu hii nimeitoa kwenye kitabu cha ndugu yetu kipenzi ‘Iswaam Jaad (Allaah Amhifadhi).  Ni kitabu chenye faida kubwa katika Nyanja ya Fiqhi ya Viapo.  Kwa hakika nimefaidika sana na kitabu hicho].

 

  الأَيْمَانُ  katika lugha ni wingi wa اليَمِيْنُ , na asili yake katika lugha ni mkono.   Kisha neno likatumika kwa maana ya kiapo, kwa kuwa watu walipokuwa wanaapizana,  kila mmoja kati yao alikuwa akigonganisha mkono wake wa kulia kwa mkono wa kulia wa mwenzake.  [Lisaanul ‘Arab na An-Nihaayatu cha Ibn Al-Athiyr].

 

 

Na اليَمِينُ katika sharia (kiistilahi), ni kuthibitisha kitu [au jambo] kwa kutaja Jina au Sifa ya Allaah.  [Fat-hul Baariy (11/516)]

 

 

                                                           

Share