003-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Viapo Vya Waislamu

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ

 

Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

03- Viapo Vya Waislamu

 

 Alhidaaya.com

 

 

Viapo ambavyo Waislamu wanaviapa na ambavyo vinaweza kuambatana na hukmu za kisharia, tunaweza kuvijumuisha katika aina mbili:  [Al-Mabsuwtw (8/126).  Angalia pia Majmuw’ul Fataawaa (35/241)].

 

 

1-  الْقَسَمُ “Kiapo”: Hiki ni kile ambacho mwenye kuapa anakusudia kwacho kumtukuza mwenye kuapiwa, na aina hii haifai isipokuwa kwa Allaah Ta’aalaa tu, kwani Yeye Ndiye Mstahiki wa Kutukuzwa kwa Dhati Yake kwa namna ambayo haijuzu kuvunja hishma ya Jina Lake kwa hali yoyote.

 

 

2-  الشَّرْطُ وَالْجَزَاءُ “Sharti na Jazaa” (yaani sharti na tokeo lake, kwa maana ya kufungamanisha tendo na uwepo wa kitu au kutokuwepo kwake).  Hili kwa mujibu wa Fuqahaa ni kiapo kwa kuwa linabeba maana ya kiapo ijapokuwa wabobezi wa lugha hawaitambui maana hii.  Kati ya viapo vya aina hii ni pamoja na yamini ya nadhiri, yamini ya talaka, yamini ya kufanya la haramu, yamini ya dhwihaar na mfano wake.

 

 

Katika mlango huu, tutaiangalia kwa kina zaidi aina ya kwanza na baadhi ya picha za aina ya pili.  Picha zake zilizobaki zimetajwa katika mahala mbalimbali husika katika Vitabu vya Fiqh.

 

 

Share