04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji:‘Aqiyqah (Akika): Je, Mnyama Mwingine Anaweza Kutosheleza Badala Ya Kondoo Au Mbuzi?

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

 

العَقِيْقَةُ

 

‘Aqiyqah (Akika)

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

04-‘Aqiyqah (Akika): Je, Mnyama Mwingine Anaweza Kutosheleza Badala Ya Kondoo Au Mbuzi?

 

Ibn Mulaykah amesema: 

 

"نُفِسَ لِعَبْدِ الرَّحْمنِ بن أَبِيْ بَكْرِ غُلَامٌ ، فَقِيْلَ لِعَائِشَةَ: يا أُمِّ المُؤْمِنِيْنَ ، عُقِّيْ عَنْهُ جَزُوْرًا ، فَقَالَتْ: مَعَاذَ اللهِ ، وَلكِن مَا قَالَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ"

 

“’Abdurrahmaan bin Abi Bakr aliruzukiwa mtoto wa kiume.  ‘Aaishah akaambiwa:  Ee Mama wa Waumini!  Mfanyie ‘aqiyqah ya ngamia.  Akasema:  Najilinda kwa Allaah, lakini (nitachinja) kwa mujibu wa alivyosema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):  Kondoo wawili wenye umri sawa”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imetajwa nyuma kidogo].

 

Na kundi la baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kwamba achio la kutoainisha aina ya mnyama katika kauli yake Rasuli فَأَهْرِيقُوا عَنْهُ دَمًا “Basi mwageni damu kwa niaba yake”, linaainishwa na kauli yake nyingine:

 

"عَنِ اَلْغُلَامِ شَاتَانِ مُكَافِئَتَانِ ، وَعَنْ اَلْجَارِيَةِ شَاةٌ "

 

“Mtoto wa kiume huchinjiwa kondoo wawili wenye umri sawa, na binti kondoo mmoja”.  Na kwa muktadha huu, ‘aqiyqah haijuzu ila kwa kondoo au mbuzi tu.

 

Na mnyama anayechinjwa ni lazima asiwe na kasoro yoyote inayozuia chinjo hili la kiibada.  Lakini Ibn Hazm amesema kwenye kitabu chake cha Al-Muhallaa:  “Anatosheleza katika ‘aqiyqah mnyama mwenye kasoro, ni sawa kasoro zinazojuzisha kwa mnyama wa udhwhiyah, au zile zisizojuzisha, lakini aliyekamilisha vigezo ni bora zaidi”.  

 

Ninasema:  “Linatosha Neno Lake Ta’aalaa:

 

"وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ"

 

“Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa”.  [Al-Baqarah: 267]

 

Na kauli yake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"إِنَّ اللَّهَ طَيِّبٌ لَا يَقْبَلُ إِلَّا طَيِّبًا"

 

“Hakika Allaah Ni Mzuri na Hakubali isipokuwa kilicho kizuri tu”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (1015) na wengineo].

                                                                                   

 

 

 

 

 

Share