01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: (Vinywaji) Taarifu Yake Na Asili Ya Uhalali Wake
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا
Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi
الأَشْرِبَةُ
Vinywaji
01- Vinywaji: Taarifu Yake Na Asili Ya Uhalali Wake:
Vinywaji "الأَشْرِبَةُ" , ni wingi wa "شَرَابُ" kinywaji, na "الشَّرَابُ" ni jina la chochote kinachonywewa kwa aina yake yoyote kiwavyo, ni sawa yawe maji au kinginecho, na kwa hali yoyote kiwavyo, na kila kitu kisichotafunwa, basi husemwa kuwa kinanywewa. [Lisaanul ‘Arab na Mukhtaar As-Swihaah].
· Asili Ya Vinywaji Vyote Ni Halali Ila Vile Vilivyoharamishwa Na Qur-aan Au Hadiyth:
Ni kwa ujumuishi wa dalili zilizotajwa kwenye mlango wa vyakula nyuma zinazothibitisha uasili wa uhalali, lakini pia kwa Hadiyth ya Anas bin Maalik (Radhwiya Allaah ‘anhu):
" لَقَدْ سَقَيْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِهَذَا الْقَدَحِ الشَّرَابَ كُلَّهُ، الْمَاءَ، وَالنَّبِيذَ، وَالْعَسَلَ، وَاللَّبَنَ"
“Kwa hakika nilimnywesha Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) vinywaji vyote kwa kikombe hiki; maji, juisi ya zabibu, asali, na maziwa”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2008) na At-Tirmidhiy katika Ash-Shamaail (1/294)].