09-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: (Vinywaji) Nabidh "النَّبِيْذُ" Itokanayo Na Aina Moja

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

 

الأَشْرِبَةُ

 

Vinywaji 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

009- Vinywaji: Nabidh "النَّبِيْذُ" Itokanayo Na Aina Moja:

 

[Al-Mudawwanah (6/263), Rawdhwat At-Twaalibiyna (10/168), Al-Mughniy na Fat-hul Baariy (10/57)].

 

"النَّبِيْذُ" (Nabiydh), ni tende kavu (tamr) au zabibu kavu au mfano wa viwili hivi ambavyo hulowekwa ndani ya maji mpaka maji hayo yakageuka tamu na kupata ladha ya vitu hivyo, kisha hunywewa.  Maji hayo (juisi) yanakuwa halali kunywewa ikiwa muda wa kulowekwa ni mfupi au mdogo kiasi cha kutokuwa makali au ya kulewesha.

 

Ama muda wa kulowekwa, Mahanbali wamesema ni siku moja na usiku wake.    Ama Wamaalik na Mashaafi’iy, wao muda hawakuuzingatia, wanachoangalia ni kinywaji kufikia nguvu ya kulewesha au la.  Nami ninasema kwamba hili ndilo linalokubalika zaidi.  Kijakazi wa Kihabeshi amesema:

 

"كُنْتُ أَنْبِذُ للنَّبِيِّ فِيْ سِقَاءٍ مِنَ اللَّيْلِ وَأُوْكِيْهِ وَأُعَلِّقُهُ، فَإِذَا أَصْبَحَ شَرِبَ مِنْهُ"

 

“Nilikuwa nikimtengenezea Rasuli juisi ya (tende au zabibu kavu) kwenye kiriba cha ngozi kuanzia usiku, nikakifunga mdomo wake na kukitundika, na kunapopambazuka anainywa”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2005)].   

 

Ibn ‘Abbaas amesema:

 

"كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُنْتَبَذُ لَهُ أَوَّلَ اللَّيْلِ فَيَشْرَبُهُ إِذَا أَصْبَحَ يَوْمَهُ ذَلِكَ ، وَاللَّيْلَةَ الَّتِي تَجِيءُ ، وَالْغَدَ ، وَاللَّيْلَةَ الأُخْرَى ، وَالْغَدَ إِلَى الْعَصْرِ، فَإِنْ بَقِيَ شَىْءٌ سَقَاهُ الْخَادِمَ ، أَوْ أَمَرَ بِهِ فَصُبَّ" 

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akilowekewa zabibu kavu (au tende kavu) mwanzoni mwa usiku, kisha hunywa maji yake tamu inapopambazuka siku yake yote na usiku wake ujao, na kesho pamoja na usiku wake, na siku inayofuatia hadi alasiri.  Kama kitabakia chochote, basi humpa mtumishi wake anywe, au huamuru yakamwagwa”.   [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (2004)].

 

 

Share