018-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Kutumia Manukato Mazuri
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ وَأَحْكَامُ النَّظَرِ
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ
Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume
018- Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Kutumia Manukato Mazuri:
Kutumia manukato (mafuta) mazuri kwa mwanaume ni katika mapambo yenye kupendelewa. Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"إِنَّ خَيْرَ طِيبِ الرِّجَالِ مَا ظَهَرَ رِيحُهُ وَخَفِيَ لَوْنُهُ ، وَخَيْرَ طِيبِ النِّسَاءِ مَا ظَهَرَ لَوْنُهُ وَخَفِيَ رِيحُهُ"
“Hakika manukato bora zaidi kwa wanaume ni yale yenye kusikika harufu, yasiyoonekana rangi yake, na manukato bora zaidi kwa wanawake ni yale yenye kuonekana rangi yake, yasiyosikika harufu”. [Hasanun Lighayrih. Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (2788) na Abu Daawuwd (2174)].
Toka kwa ‘Aaishah:
"كُنْتُ أُطَيِّبُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِأَطْيَبِ مَا نَجِدُ حَتَّى أَجِدَ وَبِيصَ الطِّيبِ فِي رَأْسِهِ وَلِحْيَتِهِ"
“Nilikuwa nikimtia Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mafuta mazuri zaidi tunayokuwa nayo mpaka naona mng’ao wa mafuta kwenye kichwa chake na ndevu zake”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5923) na Muslim (1190)].
Ibn Battwaal amesema: “Tunafahamu kutokana na Hadiyth hii kwamba mwanaume hapaki mafuta mazuri usoni mwake kinyume na akina mama. Akina mama kwa maumbile yao hujipodoa nyuso zao na kujiremba kwa mafuta hayo na mengine kinyume na akina baba. Mwanaume haruhusiwi kisharia kujitia mafuta usoni ili asije kujifananisha na wanawake”. [Al-Fat-hu (10/366)].
Na kama alivyosema Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
"أَطْيَبُ الطِّيبِ الْمِسْكُ"
“Manukato mazuri zaidi ni miski”. [Hadiyh Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2252)].
· Usikatae Mafuta Mazuri Ukipewa
Anas alikuwa hakatai mafuta mazuri, na amesema:
"أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ لَا يَرُدُّ الطِّيبَ"
“Kwamba Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa hakatai mafuta mazuri”. [Hadiyh Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (5929), na mfano wake iko kwenye Swahiyhul Jaami’i (4852)].
Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alahyi wa aalihi wa sallam) amesema:
"مَنْ عُرِضَ عَلَيْهِ رَيْحَانٌ فَلَا يَرُدُّهُ فَإِنَّهُ خَفِيفُ الْمَحْمَلِ طَيِّبُ الرّيح"
“Atakayetunukiwa rayhani basi asiikatae, kwa kuwa inabebeka kirahisi, ina harufu njema”. [Hadiyh Swahiyh. Imekharijiwa na Muslim (2253), Abu Daawuwd, An-Nasaaiy, kwao iko “Twiyb” badala ya “Rayhani”].