01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Kivazi Cha Mwanamke: Kivazi Cha Mwanamke Mbele Ya Wanaume Wasio Maharimu
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
كِتابُ اللِّباسِ وَالزِّينَةِ وَأَحْكامِ النَّظَر
Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia
لِبَاسُ المَرْأَةِ
Kivazi Cha Mwanamke
001-Kivazi Cha Mwanamke Mbele Ya Wanaume Wasio Maharimu
(a) Ni haramu kujishaua kwa kuonyesha uzuri wake na mapambo, na hili limetolewa makamio makali. Allaah Amelikataza hili kwa kusema:
"وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَىٰ"
“Na wala msionyeshe mapambo na uzuri kwa ajinabi mkajishaua kama zama za ujahili”. [Al-Ahzaab: (33)].
Umaymah bint Ruqayqah alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kupeana naye ahadi ya fungamano la Uislamu. Rasuli akamwambia:
"أُبَايِعُكِ على أَنْ لا تُشْرِكِيْ باللهِ شَيْئًا ، ولاَ تَسْرِقِيْ ، ولا تَزْنِيْ ، ولا تَقْتُلِيْ وَلَدَكَ ، ولا تَاْتِي بِبُهْتَانٍ تَفْتَرِيْنَهُ بَيْنَ يَدَيْكِ وَرِجْلَيْكِ ، ولا تَنُوْحِيْ ، ولا تَبَرَّجِيْ تَبَرُّجَ الجَاهِلِيَّةِ الأُوْلَى"
“Ninachukua ahadi ya fungamano kwako kwamba hutomshirikisha Allaah na chochote, wala hutoiba, wala hutozini, wala hutoua watoto wako, wala hutoleta uzushi wowote ukauzua baina ya mikono yako na miguu yako, wala hutoomboleza kijahili, wala hutojishaua mshauo wa ujahili wa kale”. [Musnad Ahmad (2/192) kwa Sanad Hasan].
Naye Abu Hurayrah amehadithia akisema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
"صِنْفَانِ مِنْ أَهْلِ النَّارِ لَمْ أَرَهُمَا: قَوْمٌ مَعَهُمْ سِيَاطٌ كَأَذْنَابِ الْبَقَرِ يَضْرِبُونَ بِهَا النَّاسَ ، وَنِسَاءٌ كَاسِيَاتٌ عَارِيَاتٌ مُمِيلَاتٌ مَائِلَاتٌ رُؤُوْسُهُنَّ كَأَسْنِمَةِ الْبُخْتِ الْمَائِلَةِ ، لَا يَدْخُلْنَ الْجَنَّةَ وَلَا يَجِدْنَ رِيحَهَا ، وَإِنَّ رِيحَهَا لَتُوجَدُ مِنْ مَسِيرَةِ كَذَا وَكَذَا"
“Sampuli mbili za watu wa motoni sijaziona bado: Watu wenye mijeledi mithili ya mikia ya ng’ombe wanawapiga nayo watu (bila haki), na wanawake waliovaa lakini kiuhalisia wako uchi, wanawashawishi wenzao kuwa kama wao (au kuwasisimua wanaume), na wanatembea kwa maringo wakipindisha mabega yao, vichwa vyao ni kama nundu za ngamia zilizoinama. Hao hawaingii Peponi na hawatoipata harufu yake, na kwa hakika harufu yake inasikika toka mwendo kadha wa kadha”. [Swahiyh Muslim (2128)].