07-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Kivazi Cha Mwanamke: Mwanamke Anaruhusiwa Kuvaa Hariri

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

لِبَاسُ المَرْأَةِ

Kivazi Cha Mwanamke 

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

007- Mwanamke Anaruhusiwa Kuvaa Hariri:

 

Jua dada yangu Muislamu kwamba wanawake wanaruhusiwa kuvaa hariri lakini wanaume hawaruhusiwi kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"حُرِّمَ لِبَاسُ الْحَرِيرِ وَالذَّهَبِ عَلَى ذُكُورِ أُمَّتِي وَأُحِلَّ لإِنَاثِهِمْ"

 

“Kuvaa hariri na dhahabu kumeharamishwa kwa wanaume wa umati wangu, lakini kumehalalishwa kwa wanawake wao”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4057), At-Tirmidhiy (1720), An-Nasaaiy (8/160) na Ibn Maajah (3595)].

 

‘Aliyy amesema:

 

"كَسَانِي اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حُلَّةً سِيَرَاءَ، فَخَرَجْتُ فِيهَا، فَرَأَيْتُ اَلْغَضَبَ فِي وَجْهِهِ، فَشَقَقْتُهَا بَيْنَ نِسَائِي" 

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alinivisha vazi la “siyraa”, nami nikatoka nalo nje nimelivaa, nikaona ghadhabu kwenye uso wake, nikalipasua, nikaligawa kati ya wake (wa jamaa) zangu”.  [Al-Bukhaariy (5840) na Muslim (2071)].

 

Ametoa dalili kwa maneno haya kwamba inajuzu kwa mwanamke kuvaa hariri safi asili kwa kujengea kwamba vazi la “siyraa” halishonwi ila kwa hariri safi.  [Fat-hul Baariy (1/300)].

 

 

 

Share