01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanaume Asiye Maharimu Kumwangalia Mwanamke

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com 

 

 

 

01-Mwanaume Asiye Maharimu Kumwangalia Mwanamke:

 

Ni haramu kwa mwanaume kumwangalia mwanamke bila dharura, na Allaah Amewaamuru kuinamisha macho yao chini.

 

1-  Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ۚ ذَٰلِكَ أَزْكَىٰ لَهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا يَصْنَعُونَ ﴿٣٠﴾

 

30.  Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao. Hivyo ni utakaso zaidi kwao.  Hakika Allaah Ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale wayatendayo.  [An-Nuwr: 30] 

 

 

2-  Ibn ‘Abbaas amesema:

 

"كَانَ الْفَضْلُ بْنُ عَبَّاسٍ رَدِيفَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ، فَجَاءَتْهُ امْرَأَةٌ مِنْ خَثْعَمَ تَسْتَفْتِيهِ ، فَجَعَلَ الْفَضْلُ يَنْظُرُ إِلَيْهَا وَتَنْظُرُ إِلَيْهِ ، فَجَعَلَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَصْرِفُ وَجْهَ الْفَضْلِ إِلَى الشِّقِّ الآخَرِ"

 

“Al-Fadhl bin ‘Abbaas alikuwa amepanda nyuma ya mnyama wa Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam), akamjia mwanamke toka Khath-’am kumuuliza fatwa.  Al-Fadhl akaanza kumwangalia mwanamke huyo, na mwanamke naye akawa anamwangalia.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaugeuza uso wa Fadhl akauelekeza upande mwingine”.  [Al-Bukhaariy (6228) na Muslim (1218)]

 

Kitendo hiki cha Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kinamaanisha kuzuia na kukataza kufanya hivyo kwa mwanaume.

 

3-  Jariyr bin ‘Abdullaah amesema:

 

"سَأَلَتْ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ نَظَرِ الْفُجَاءَةِ ، فَأَمَرَنِي أَنْ أَصْرِفَ بَصَرِي"

 

“Nilimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kuangalia kwa ghafla.  Akaniamuru nigeuze jicho langu sehemu nyingine”.   [Muslim (2109), Abu Daawuwd (2148) na At-Tirmidhiy (2776)]

 

4-   Ibn Buraydah toka kwa baba yake amesema:  “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia ‘Aliyy:

 

"يَا عَلِيُّ لاَ تُتْبِعِ النَّظْرَةَ النَّظْرَةَ فَإِنَّ لَكَ الأُولَى وَلَيْسَتْ لَكَ الآخِرَةُ ‏"

 

“Ee ‘Aliyy!  Ukiangalia mara moja, usiongeze tena na tena, kwa la kwanza hulaumiwi, lakini jingine hapana”.  [At-Tirmidhiy (2777), Abu Daawuwd (2149), na Ahmad (1377).  Sanad yake ni Hasanun Lighayrih]

 

 

Share