04-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Hukumu Za Kuangalia: Mwanamke Anaweza Kuangaliwa na Hakimu Na Shahidi Na Katika Miamala

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

  

أَحْكَامُ النَّظَرِ

Hukumu Za Kuangalia 

  

Alhidaaya.com 

 

                                                                       

04-Mwanamke Anaweza Kuangaliwa na Hakimu Na Shahidi Na Katika Miamala:

 

Hakimu na shahidi kumwangalia mwanamke ni katika hali zinazovuliwa kwa dharura.  Na hii ni pale anapoitwa mwanaume kumtolea mwanamke ushahidi wa kumtoa kwenye tuhuma au kumthibitishia.   Au hakimu akiwa mwanaume itabidi amtazame ili atoe hukumu ya adhabu likithibiti kosa kama atakiri au kumwachia,  au kwa mashuhuda kutoa ushahidi wa kwamba wanamjua na kadhalika.  Hii ni kwa vile katika kesi ni lazima mwanamke atazamwe ili hukumu iwe ya haki.  Mambo ya dharura huhalalisha yaliyo marufuku. 

 

Na ikiwa shahidi atamtambua akiwa na niqab, basi si lazima afunue, kwa kuwa dharura hukadiriwa kwa kiasi chake.

 

Kumwangalia Kwa Ajili Ya Muamala Kama Kuuza Au Kununua:

 

Fuqahaa wanasema kwamba inajuzu mwanaume kumwangalia mwanamke kwa ajili ya muamala kama biashara na kadhalika.  Mwanaume akifanya biashara na mwanamke kwa kununua kutoka kwake au kumuuzia, ni lazima amwangalie na amjue vizuri -lakini kwa kadiri ya haja- ili kudhamini haki yake ya malipo au thamani ya bidhaa au haki nyingine yoyote inayohusiana na biashara kati yao.  

 

An-Nawawiy amesema:  “Inajuzu kwa mwanaume kuangalia uso wa mwanamke ajnabiya wakati wa kutoa ushahidi, na wakati wa kuuza au kununua kutoka kwake.  Na yeye anaruhusiwa vile vile kuangalia uso wa mwanaume”.  [Al-Majmuw’u (16/139)].

 

 

Share