020-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ipi Dalili Kuthibitisha Masharti Hayo Kupitia Qur-aan Na Sunnah?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
020-Ipi Dalili Kuthibitisha Masharti Hayo Kupitia Qur-aan Na Sunnah?
Swali:
س: ما دليل اشتراط العلم من الكتاب والسنة
Ipi dalili kuthibitisha masharti hayo kupitia Qur-aan na Sunnah?
Jibu:
ج: قول الله تعالى ( إلا من شهد بالحق ) أي بلا إله إلا الله ( وهم يعلمون ) بقلوبهم معنى ما نطقوا به بألسنتهم وقول النبي صلى الله عليه وسلم ( من مات وهو يعلم أن لا إله إلا الله دخل الجنة )
Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى) Anayosema:
إِلَّا مَن شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٨٦﴾
isipokuwa yule aliyeshuhudia kwa haki, nao wanaju. [Az-Zukhruf (43:86)]
Maana yake ni kwamba: Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali wakijua.
Kukiri kwa nyoyo zao ina maana hawakutamka kwa ndimi zao.
Na kauli ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema:
مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ
((Mwenye kufa na hali anajua kuwa laa ilaaha illa-Allaah ataingia peponi)) [Muslim na Ahmad]