027-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Kupenda Kwa Ajili Ya Allaah Na Kuchukia Kwa Ajili Yake?

 

 

 200سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ 

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)  

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

027-Ni Ipi Dalili Ya Kupenda Kwa Ajili Ya Allaah Na Kuchukia Kwa Ajili Yake? 

 

Swali:

س: ما دليل الموالاة لله والمعاداة لأجله 

 

Ni ipi dalili ya kupenda kwa ajili ya Allaah na kuchukia kwa ajili Yake?

 

Jibu:

 

ج: قال الله عز وجل( يا أيها الذين آمنوا لا تتخذوا اليهود والنصارى أولياء بعضهم أولياء بعض ومن يتولهم منكم فإنه منهم )إلى قوله( إنما وليكم الله ورسوله والذين آمنوا )إلى آخر الآيات. وقال تعالى( يا أيها الذين آمنوا لا تتخذوا آباءكم وإخوانكم أولياء إن استحبوا الكفر على الإيمان )الآيتين. وقال تعالى( لا تجد قوما يؤمنون بالله واليوم الآخر يوادون من حاد الله ورسوله )الآية. وقال تعالى( يا أيها الذين آمنوا لا تتخذوا عدوي وعدوكم أولياء )إلى آخر السورة وغير ذلك من الآيات.

 

Ni kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَىٰ أَوْلِيَاءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٥١﴾

Enyi walioamini! Msifanye Mayahudi na Manaswara marafiki wandani na walinzi. Wao kwa wao ni marafiki wandani. Na yeyote atakayewafanya marafiki wao wandani, basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu.

فَتَرَى الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ يُسَارِعُونَ فِيهِمْ يَقُولُونَ نَخْشَىٰ أَن تُصِيبَنَا دَائِرَةٌ ۚ فَعَسَى اللَّـهُ أَن يَأْتِيَ بِالْفَتْحِ أَوْ أَمْرٍ مِّنْ عِندِهِ فَيُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا أَسَرُّوا فِي أَنفُسِهِمْ نَادِمِينَ ﴿٥٢﴾

Utawaona wale ambao katika nyoyo zao mna maradhi (ya unafiki) wanakimbilia kwao wakisema: Tunakhofu usitusibu mgeuko. Basi asaa Allaah Akaleta ushindi au jambo (jengine) litokalo Kwake, wakawa wenye kujuta kwa waliyoyaficha katika nafsi zao.

وَيَقُولُ الَّذِينَ آمَنُوا أَهَـٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمُوا بِاللَّـهِ جَهْدَ أَيْمَانِهِمْ ۙ إِنَّهُمْ لَمَعَكُمْ ۚ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فَأَصْبَحُوا خَاسِرِينَ ﴿٥٣﴾

Na hapo walioamini watasema (wanafiki wakifichuka): Je, hawa ndio wale ambao waliapa kwa Allaah kwa viapo vyao thabiti vya nguvu, kwamba wao wapo pamoja nanyi? Zimeporomoka amali zao, na wamekuwa wenye kukhasirika.

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللَّـهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَلَا يَخَافُونَ لَوْمَةَ لَائِمٍ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٥٤﴾

Enyi walioamini! Yeyote atakayeritadi miongoni mwenu akaacha Dini yake, basi Allaah Ataleta watu (badala yao) Atakaowapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waumini, washupavu juu ya makafiri, wanafanya Jihaad katika Njia ya Allaah na wala hawakhofu lawama za mwenye kulaumu. Hiyo ni Fadhila ya Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote. 

إِنَّمَا وَلِيُّكُمُ اللَّـهُ وَرَسُولُهُ وَالَّذِينَ آمَنُوا الَّذِينَ يُقِيمُونَ الصَّلَاةَ وَيُؤْتُونَ الزَّكَاةَ وَهُمْ رَاكِعُونَ ﴿٥٥﴾

Hakika Rafiki wenu Mlinzi ni Allaah na Rasuli Wake na wale walioamini, ambao wanasimamisha Swalaah na wanatoa Zakaah hali ya kuwa wananyenyekea. [Al-Maaidah: (5:51-55)]

 

Na Allaah Amesema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا آبَاءَكُمْ وَإِخْوَانَكُمْ أَوْلِيَاءَ إِنِ اسْتَحَبُّوا الْكُفْرَ عَلَى الْإِيمَانِ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ﴿٢٣﴾

Enyi walioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu marafiki wandani ikiwa wanapendelea ukafiri badala ya imaan. Na atakayewafanya marafiki wandani miongoni mwenu, basi hao ndio madhalimu. [At-Tawbah: (9:23)]

 

Na Allaah Akasema tena:

 

 

لَّا تَجِدُ قَوْمًا يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ يُوَادُّونَ مَنْ حَادَّ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَلَوْ كَانُوا آبَاءَهُمْ أَوْ أَبْنَاءَهُمْ أَوْ إِخْوَانَهُمْ أَوْ عَشِيرَتَهُمْ ۚ ﴿٢٢﴾

Hutokuta watu wanaomuamini Allaah na Siku ya Mwisho kuwa wanafanya urafiki na kuwapenda wanaompinga Allaah na Rasuli Wake, japo wakiwa ni baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au jamaa zao. [Al-Mujaadalah: (58:22)]

 

Na Aayah nyingine Allaah Anasema:

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ ﴿١﴾

Enyi walioamini! Msifanye adui Wangu na adui wenu kuwa marafiki  [Al-Mumtahinah: (60:1)]

 

 

Na Aayah nyenginezo.

 

Share