032-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Dalili Ya Swaum?
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
032-Ni Ipi Dalili Ya Swaum?
Swali:
س: ما دليل الصوم
Ni ipi dalili ya Swaum?
Jibu:
ج: قال الله تعالى( يا أيها الذين آمنوا كتب عليكم الصيام كما كتب على الذين من قبلكم )وقال تعالى( فمن شهد منكم الشهر فليصمه ) الآيات, وفي حديث الأعرابي: أخبرني ما فرض الله علي من الصيام. فقال( شهر رمضان إلا أن تطوع شيئا )الحديث.
Ni kauli ya Allaah(سبحانه وتعالى):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٨٣﴾
Enyi walioamini! Mmefaridhishwa Swiyaam kama ilivyofaridhishwa kwa walio kabla yenu mpate kuwa na taqwa. [Al-Baqarah: (2:183)]
Na kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):
فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ ۖ ﴿١٨٥﴾
Kwa hiyo atakayeshuhudia miongoni mwenu mwezi na afunge. [Al-Baqarah: (2:185)]
Na katika kauli ya Bedui:
Nijulishe nini Allaah amenifaradhishia mimi kutokana na Swaum? Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamjibu:
"Amefaradhisha mwezi wa Ramadhwaan, isipokuwa kujitolea (Swaum ya Sunnah)".