01-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Himizo Na Raghibisho La Kuoa

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

 

 

01-Himizo Na Raghibisho La Kuoa:

 

1-  Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا رُسُلًا مِّن قَبْلِكَ وَجَعَلْنَا لَهُمْ أَزْوَاجًا وَذُرِّيَّةً"

 

“Na kwa yakini Tulituma Rusuli kabla yako, na Tukawajaalia wawe na wake na dhuria”.  [Ar-Ra’ad: 38]

 

2-  Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"وَأَنكِحُوا الْأَيَامَىٰ مِنكُمْ وَالصَّالِحِينَ مِنْ عِبَادِكُمْ وَإِمَائِكُمْ"

 

“Na waozesheni wajane miongoni mwenu na walio Swalihina kati ya watumwa  wenu wanaume na wajakazi wenu”.  [An-Nuwr: 32]

 

3-  Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ"

 

“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne”.  [An-Nisaa: 03]

 

4-  Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ"

 

Na katika Ishara Zake ni kwamba Amekuumbieni katika jinsi yenu wake ili mpate utulivu kwao, na Amekujaalieni baina yenu mapenzi na rahmah.  Hakika pana katika hayo, bila shaka mazingatio kwa watu wanaotafakari”.  [Ar-Ruwm: 21]

 

5-  Hadiyth ya Anas kuhusiana na kisa cha watu watatu ambao:

 

"قَالَ أَحَدُهُمْ: أَمَا أَنا فَإِنِّي أُصَلِّي اللَّيْلَ أَبَدًا، وَقَالَ آخَرُ: أَنا أَصُومُ الدَّهْرَ وَلَا أُفْطِرُ، وَقَالَ آخرُ: أَنَا أَعْتَزِلُ النِّسَاءَ فَلَا أَتَزَوَّجُ أَبَدًا، فَجَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَيْهِمْ فَقَالَ: أَنْتُمُ الَّذِينَ قُلْتُمْ كَذَا وَكَذَا، أَمَا وَاللَّهِ إِنِّي لَأَخْشَاكُمْ لِلَّهِ وَأَتْقَاكُمْ لَهُ، لَكِنِّي أَصُومُ وَأُفْطِرُ، وَأُصَلِّي وَأَرْقُدُ، وَأَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي"

 

“Mmoja wao alisema:  Ama mimi, hakika nitaswali siku zote swalaah za usiku.  Na mwingine akasema:  Mimi nitafunga mwaka mzima na sitokula mchana.  Na wa tatu akasema:  Mimi nitakaa mbali na wanawake, sitooa abadan.  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaja na kuwauliza:  Nyinyi ndio mliosema kadha wa kadha?  Naapa kwa Allaah kwa ukweli kwamba mimi ndiye ninayemwogopa na kumcha zaidi Allaah kuliko nyinyi nyote, lakini ninafunga na ninakula mchana, ninaswali na ninalala, na ninaoa wanawake.  Basi yeyote atakayejiengua na njia na mwenendo wangu, basi huyo yuko mbali nami”.  [Hadiyth Swahiyh.  Al-Bukhaariy (5063) na Muslim (1401)]

 

6-  Ma’aqil bin Yasaar:  “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"تَزَوَّجُوا الْوَدُودَ الْوَلُودَ فَإِنِّي مُكَاثِرٌ بِكُمُ الْأُمَم"

 

“Oeni mwanamke mwenye penzi la dhati, mwenye rutuba ya kizazi, kwani mimi nitajifakhiri kwa wingi wenu mbele ya umma zilizotangulia (Siku ya Qiyaamah)”.  [Swahiyh.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2050), An-Nasaaiy (6/65) na wengineo]

 

7-  Ibn Mas-‘uwd:  “Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alituambia:

 

"يَا مَعْشَرَ الشَّبَابِ، مَنِ اسْتَطَاعَ مِنْكُمُ الْبَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ ، وَمَنْ لَمْ يَجِدْ فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ فَإِنَّهُ لَهُ وِجَاءٌ"

 

“Enyi rika la vijana!  Atakayeweza gharama za kuolea miongoni mwenu basi aoe, kwani kuoa kunaliinamisha jicho na kunailinda tupu, na ambaye hatoweza, basi afunge, kwani funga kwake ni kata kiu ya matamanio ya jimai”.  [Hadiyth Swahiyh.  Al-Bukhaariy (5065) na Muslim (1400)]

 

8-  Abu Dharr:  “Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"وَفِي بُضْعِ أَحَدِكُمْ صَدَقَةٌ، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَيَأْتِي أَحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أَجْرٌ؟ قَالَ: أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَهَا فِي حَرَامٍ أَكَانَ عَلَيْهِ فِيهِ وِزْرٌ؟ فَكَذَلِكَ إِذَا وَضَعَهَا فِي الْحَلَالِ كَانَ لَهُ أَجْرٌ"

 

“Na mmoja wenu akimuingilia mkewe anapata pia thawabu.  Wakauliza:  Ee Rasuli wa Allaah!  Inakuwaje mmoja wetu akidhi matamanio yake halafu apate na thawabu juu!?  Akawaambia:  Niambieni, itakuwaje kama atayaweka katika haramu, je, si atapata madhambi kwa kufanya hivyo?  Ndivyo hivyo hivyo, akiyaweka kwenye halali, basi anapata thawabu pia ”.  [Hadiyth Swahiyh.   Imekharijiwa na Muslim (1006) na Abu Daawuwd (1286)]    

 

9-  ‘Abdullaah bin ‘Amri:  “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"الدُّنْيَا مَتَاعٌ، وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَةُ"

 

“Dunia ni starehe, na starehe bora zaidi ya dunia ni mwanamke mwema”.  [Hadiyth Swahiyh.  Muslim (1467)]

 

10-  Sa’iyd bin Jubayr:  “Ibn ‘Abbaas aliniuliza: 

 

"هَلْ تَزَوَّجْتَ؟ قُلْتُ: لاَ‏.‏ قَالَ: فَتَزَوَّجْ، فَإِنَّ خَيْرَ هَذِهِ الأُمَّةِ أَكْثَرُهَا نِسَاءً‏"

 

“Je una mke?  Nikamwambia sina.  Akaniambia:  Basi oa, kwani mbora wa umma huu (Rasuli Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndiye aliyeoa wake wengi zaidi”.  [Isnaad yake ni Swahiyh]

 

 

Share