22-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mwanamke Wa Kiislamu Ni Haramu Kuolewa Na Kafiri

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

 

 

22-Mwanamke Wa Kiislamu Ni Haramu Kuolewa Na Kafiri:

 

 

Hii ni sawa ikiwa mwanaume ni katika Ahlul Kitaab au dini nyingine kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:

 

"وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ"

 

“Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini.  Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni.  Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini.  Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni.  Hao wanaitia katika moto na Allaah Anaitia katika Jannah na maghfirah kwa Idhini Yake”.  [Al-Baqarah: 221]

 

 

Share