043-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Nini Maana Ya Kumuamini Allaah ('Azza wa Jalla)
200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة
Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah
لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ
Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)
Imefasiriwa na: Alhidaaya.com
043-Nini Maana Ya Kumuamini Allaah ('Azza wa Jalla)
Swali:
س: ما معنى الإيمان بالله عز وجل
Nini maana ya kumuamini Allaah ('Azza wa Jalla)?
Jibu:
ج: هو التصديق الجازم من صميم القلب بوجود ذاته تعالى الذي لم يسبق بضد ولم يعقب به هو الأول فليس قبله شيء ,والآخر فليس بعده شيء والظاهر فليس فوقه شيء والباطن فليس دونه شيء حي قيوم أحد صمد( لم يلد ولم يولد ولم يكن له كفوا أحد )وتوحيده بإلهيته وربوبيته وأسمائه وصفاته.
Ni kukubali moja kwa moja kwa moyo kwamba Allaah Yupo Ambaye Hana Mshirika, Yeye Ndie Mwanzo hakuna kabla Yake, Naye Ndie wa Mwisho hana baada Yake kitu, Yeye Ndie wa Dhahiri Hana juu Yake kitu chochote, Yeye Ndie wa Siri Hana ndani Yake kitu chochote, Yu Hai, Msimamizi, wa Pekee, Mwenye Kukusiwa, (Hakuzaa wala Hakuzaliwa. Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye). Na kumpwekesha Yeye kwa Uungu Wake na usimamizi Wake, pamoja na majina Yake na Sifa Zake.