048-Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah: Ni Ipi Tofuati Kati ya (waw)-na Na Thumma (kisha) Katika Matamshi Haya?

 

 

200 سُؤالٌ وَ جَوَابٌ فِي الْعَقِيدَة

Maswali 200 Na Majibu Ya ‘Aqiydah

 

لِلشَّيخ حافِظ بن أحْمَد الحَكمَيّ

Shaykh Haafidhw Bin Ahmad Al-Hakamiyy (رحمه الله)

Imefasiriwa na:  Alhidaaya.com

 

048-Ni Ipi Hiyo Tofauti Kati ya (waw)-na Na Thumma (kisha) Katika Matamshi Haya?

 

 

Swali:

س: ما الفرق بين الواو وثم في هذه الألفاظ

Ni ipi tofuati kati ya (waw)-na na thumma (kisha) katika matamshi haya?

 

Jibu:

ج: لأن العطف بالواو يقتضي المقارنة والتسوية فيكون من قال ما شاء الله وشئت قارنا مشيئة العبد بمشيئة الله مسويا بها بخلاف العطف بثم المقتضية للتبعية فمن قال ما شاء الله ,ثم شئت فقد أقر بأن مشيئة العبد تابعة لمشيئة الله تعالى لا تكون إلا بعدها كما قال تعالى( وما تشاءون إلا أن يشاء الله ) وكذلك البقية.

Kwa sababu herufi ya Waw (na) inafahamisha usawa. Mfano: Mtu akisema hivi: Akipenda Allaah na wewe, inajulisha usawa kati ya mja na Allaah katika kupenda kwa pamoja. Kinyume cha Thumma inajulisha baada.

 

Mfano: Mtu akisema: Akipenda Allaah halafu wewe. Inajulisha baada ya kutaka Allaah ndio atake mja, na hapa haijulishi pamoja. 

Ni kauli ya Allaah  (عزَّ وجلَّ):

وَمَا تَشَاءُونَ إِلَّا أَن يَشَاءَ اللَّـهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمًا﴿٣٠﴾

Na hamtoweza kutaka isipokuwa Atake Allaah. Hakika Allaah daima Ni Mjuzi wa yote, Mwenye Hikmah wa yote. [Al-Insaan: (76:30)]

 

 

 

 

Share