18-Malaika: Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha: (1)- Maalik Mlinzi Na Msimamizi Wa Jahannam

 

Malaika

 

Alhidaaya.com

 

18:  Malaika Wenye Sura Na Maumbo Ya Kutisha

 

(1)-  Maalik Mlinzi Na Msimamizi Wa Jahannam

 

 

Toka kwa Samurah bin Jundub (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema akihadithia njozi yake:

 

"فانطَلَقْنا فأَتَينا على رَجُلٍ كَرِيهِ المَرْآةِ، كأكرَهِ ما أنت راءٍ رَجُلًا مَرآةً، وإذا عِنْدَه نارٌ يَحُشُّها ويسعى حَولَها. قال: قُلْتُ لهما: ما هذا؟! قال: قالا لي: انطَلِقِ انطَلِقِ، فانطَلَقْنا... -وفيه-: قالا لي:... وأمَّا الرَّجُلُ الكَريهُ المَرْآةِ، الذي عند النَّارِ يَحُشُّها ويَسْعى حَوْلَها، فإنَّه مالِكٌ خازِنُ جَهَنَّمَ"

 

“…Tukaondoka, halafu tukamjia mtu mwenye mwonekano mbaya mno, kama vile unavyomwona mtu mwenye sura mbaya mno ambayo hujapata kuiona.  Na mtu huyo ana moto anaouchochea na anakwenda akiuzunguka.  Nikawauliza: Nani huyu?  Wakaniambia:  Twende, twende, tukaondoka.  (Na Rasuli alipowauliza baadae Malaika hao wawili kuhusu mtu huyo mwenye sura mbaya mno walimwambia):  Huyo ni Maalik mlinzi wa Jahannam”.   [Hadiyth Swahiyh. Al-Bukhaariy (7047)]

 

Ibn Rajab amesema:  “Maalik ndiye mlinzi wa Jahannam, na ndiye mkuu wa walinzi wa Jahannam.  Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona usiku wa Mi’iraji”.

 

Na mwonekano wake huo mbaya, utakuwa ni nyongeza ya adhabu kwa watu wa motoni.  Allaah Atulinde nao.

 

 

 

Share