Tahadhari Kuhadithia Jambo Kisha Kumalizia Kwa Kusema: وَلَا الضَّالِّينَ

 

 

Tahadhari Kuhadithia Jambo Kisha Kumalizia Kwa Kusema:  

 

 

وَلَا الضَّالِّينَ

(Neno La Qur-aan Linalomalizika Katika Suwrah Al-Faatihah)

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

Haijuzu kutumia au kuingiza maneno ya Qur-aan katika magumzo ya mitaani na yasiyohusiana na Dini, kama vile kusema:

 

وَلَا الضَّالِّينَ

pale mtu anapotaka kumalizia kuhadithia gumzo lake.

 

 

Makosa haya yanaweza kumtoa mtu nje ya Uislamu kwa sababu kufanya istihzai (masikhara) katika yanayohusiana na Dini ya Allaah ni kukufuru!  Na dalili ni Aayah Alizoteremsha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kuwahusu watu waliofanya istihzai (masikhara) katika Dini wakadai kuwa walikuwa wanaporoja tu na kufanya mzaha. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُمْ لَيَقُولُنَّ إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ ۚ قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ﴿٦٥﴾

Na ukiwauliza, bila shaka watasema: Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza. Sema: Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Rasuli Wake?

 

لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ   

Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.

[Suwrah At-Tawbah (9:65-66)]

 

 

 

Share