26-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Kila Kiungo Cha Mtu Lazima Kitolewe Swadaqah
Hadiyth Ya 26
كُلُّ سُلامَى مِنَ النَّاسِ عليه صَدَقَةٌ
Kila Kiungo Cha Mtu Lazima Kitolewe Swadaqah
عن أَبي هُرَيْرَةَ رَضي اللهُ عنه قال: قالَ رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم: ((كُلُّ سُلامَى مِنَ النَّاسِ عليه صَدَقَةٌ، كُلُّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ: تَعْدِلُ بَيْنَ اثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وتُعينُ الرَّجُلَ في دَابَّتِهِ فَتَحْمِلُهُ عَلَيْها أو تَرْفَعُ لهُ عَلَيْها متَاَعَهُ صَدَقَةٌ، والْكَلِمةُ الطَّيِّبةُ صَدَقَةٌ، وبكُلِّ خَطْوَةٍ تَمشِيها إلى الصَّلاةِ صَدَقَةٌ، وتُمِيطُ الأَذَى عنِ الطَّرِيِق صَدَقَةٌ)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ وَمُسْلِمٌ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kila kiungo cha mtu lazima akitolee swadaqah kila siku linapochomoza jua. Kufanya uadilifu baina ya wawili ni swadaqah. Kumsaidia mtu kupanda mnyama wake kwa kumsaidia kumnyanyua au kumnyanyulia mizigo ni swadaqah. Neno zuri ni swadaqah. Na kila hatua unayotembea kuelekea Swalaah ni swadaqah, na kuondosha udhia katika njia ni swadaqah.” [Al-Bukhaariy na Muslim]