33-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Jukumu La Ushahidi Liko Kwa Yule Anayedai Na Kula Kiapo Kunamuwajibikia Yule Anayekanusha
Hadiyth Ya 33
البَيِّنَةُ على المُدَّعِى والْيَمينُ على من أَنْكَرَ
Jukumu La Ushahidi Liko Kwa Yule Anayedai
Na Kula Kiapo Kunamuwajibikia Yule Anayekanusha
عن ابن عَبَّاسٍ رضي اللُه عنهما: أن رسولَ الله صلى الله عليه وسلم قال: ((لَو يُعْطَى النَّاسُ بِدَعْوَاهُمْ لادَّعَى رِجَالٌ أموالَ قَوْمٍ ودِماءَهُمْ لَكِنِ البَيِّنَةُ على المُدَّعِى والْيَمينُ على من أَنْكَرَ)) حَدِيثٌ حَسَنٌ، رَوَاهُ الْبَيْهَقِيّ وَغَيْرُهُ هَكَذَا، وَبَعْضُهُ فِي الصَّحِيحَيْنِ
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kama watu wangelipewa kwa mujibu wa madai yao, watu wangelidai mali na damu za wenzao (uhai) lakini jukumu la ushahidi liko kwa yule anayedai na kula kiapo kunawajibika kwa yule anayekanusha (kuwa hakutenda)” [Al-Bayhaqiy na wengineo. Ni Hadiyth Hasan na baadhi yake imo katika Asw-Swahiyhayni]