36-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Atakayemuondoshea Muumini Dhiki Za Dunia, Allaah Atamuondoshea Dhiki Katika Dhiki Za Siku Ya Qiyaamah
Hadiyth Ya 36
مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ
Atakayemuondoshea Muumini Dhiki Za Dunia,
Allaah Atamuondoshea Dhiki Katika Dhiki Za Siku Ya Qiyaamah
عن أبي هُرَيْرَة رضي اللهُ عنه، عن النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قال: ((مَنْ نَفَّسَ عَنْ مُؤمِنٍ كُرْبَةً مِنْ كُرَبِ الدُّنْيا نَفَّسَ اللهُ عَنْهُ كُرْبَةً من كُرَبِ يوْمِ القيامَةِ، ومَنْ يَسَّرَ على مُعْسِرٍ يَسَّرَ اللهُ عليه في الدنْيا والآخِرَةِ، وَمَنْ سَتَرَ مُسْلِماً سَتَرَهُ الله في الدُّنْيا والآخِرَةِ واللهُ في عَوْنِ الْعَبْدِ ما كانَ الْعَبْدُ في عَونِ أخيهِ. ومَنْ سلك طَريقاً يَلْتَمِسُ فِيهِ عِلْماً سَهَّلَ اللهُ له بِهِ طَرِيقاً إلى الجنَّةِ.
وَمَا اجتَمَعَ قَوْمٌ في بَيْتٍ مِنْ بُيُوتِ اللهِ يَتْلُونَ كِتَابَ اللهِ ويَتَدَارَسُونَهُ بَيْنَهُمْ، إلا نَزَلَتْ عليهمُ السَّكِينَةُ، وغَشِيَتْهُمُ الرَّحْمَةُ، وحَفَّتهُمُ المَلائِكَةُ، وذَكَرَهُمُ اللهُ فيمَنْ عِنْدَه. وَمَنْ بَطَّأ بِه عَمَلُهُ لمْ يُسْرِعْ به نَسَبُهُ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ بهذا اللفظ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayemuondoshea Muumini dhiki katika dhiki za dunia, Allaah Atamuondoshea dhiki katika dhiki za Siku ya Qiyaamah. Na Atakayemsahilishia mwenye ugumu wa jambo, Allaah Atamsahilishia duniani na Aakhirah. Na Atakayemsitiri Muislamu, Allaah Atamsitiri duniani na Aakhirah. Na Allaah Humsaidia mja madamu mja yuko katika kumsaidia nduguye. Na Atakayetafuta njia ya kujipatia elimu, Allaah Atamsahilishia njia ya Jannah.
Na hawajumuiki watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakisoma Kitabu cha Allaah na wakasomeshana baina yao ila watateremkiwa na sakiynah (utulivu) na itawafunika rahmah, na Malaika watawazunguka, na Allaah Atawataja kwa walio Naye. Yeyote yule anayeakhirishwa na ‘amali zake (kwenda Jannah) hatoharakishwa na nasaba yake.” [Muslim kwa tamshi hili]