38-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Atakayemfanyia Uadui Kipenzi Changu Ninatangaza Vita Dhidi Yake
Hadiyth Ya 38
مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ
Atakayemfanyia Uadui Kipenzi Changu Ninatangaza Vita Dhidi Yake
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ قَال:َ مَنْ عَادَى لِي وَلِيًّا فَقَدْ آذَنْتُهُ بِالْحَرْبِ، وَمَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ عَبْدِي بِشَيْءٍ أَحَبَّ إِلَيَّ مِمَّا افْتَرَضْتُ عَلَيْهِ، وَمَا يَزَالُ عَبْدِي يَتَقَرَّبُ إِلَيَّ بِالنَّوَافِلِ حَتَّى أُحِبَّهُ، فَإِذَا أَحْبَبْتُهُ كُنْتُ سَمْعَهُ الَّذِي يَسْمَعُ بِهِ، وَبَصَرَهُ الَّذِي يُبْصِرُ بِهِ، وَيَدَهُ الَّتِي يَبْطِشُ بِهَا، وَرِجْلَهُ الَّتِي يَمْشِي بِهَا، وَإِنْ سَأَلَنِي لَأُعْطِيَنَّهُ، وَلَئِنْ اسْتَعَاذَنِي لَأُعِيذَنَّهُ)) البخاري
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Atakayemfanyia uadui kipenzi changu Ninatangaza vita dhidi yake. Mja Wangu hanikaribii na kitu chochote Ninachokipenda kama ‘amali nilizomfaridhishia. Na mja Wangu huzidi kunikaribia kwa ‘amali za Sunnah ili nimpende. Ninapompenda, huwa masikio yake yanayosikilizia, macho yake anayoonea, mikono yake anayonyoshea, miguu yake anayotembelea nayo, lau angeniomba kitu bila shaka ningempa, lau angeniomba himaya bila shaka ningelimkinga.” [Al-Bukhaariy]