42-Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah: Ee Bin Aadam! Madamu Utaniomba Na Kutaraji Kwangu Nitakughufuria
Hadiyth Ya 42
يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ
Ee Bin Aadam! Madamu Utaniomba
Na Kutaraji Kwangu Nitakughufuria
عن أنس رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وآله وسلم يَقُولُ: ((قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ مَا دَعَوْتَنِي وَرَجَوْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ عَلَى مَا كَانَ مِنْكَ وَلاَ أُبَالِي. يَا ابْنَ آدَمَ لَوْ بَلَغَتْ ذُنُوبُكَ عَنَانَ السَّمَاءِ ثُمَّ اسْتَغْفَرْتَنِي غَفَرْتُ لَكَ . يَا ابْنَ آدَمَ إِنَّكَ لَوْ أَتَيْتَنِي بِقُرَابِ الأَرْضِ خَطَايَا ثُمَّ لَقِيتَنِي لاَ تُشْرِكُ بِي شَيْئًا لاَتَيْتُكَ بِقُرَابِهَا مَغْفِرَةً)) رَوَاهُ التِّرْمِذِيُّ وَقَالَ: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Allaah Ta’aalaa Amesema: Ee bin-Aadam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakughufuria yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee bin-Aadam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfirah, Ningekughufuria (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee bin-Aadam! Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na maghfirah yanayolinga nayo.” [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]