17-Abu Bakr Asw-Swiddiyq (Radhwiya Allaahu 'anhu): Kupambana na waliortadi
Baadhi ya makabila yanayoishi mbali na mji wa Madiynah na ambayo yaliingia karibuni tu katika Uislamu, yalianza kufanya uasi na kurtadi mara baada ya kusikia habari za kifo cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Walirtadi baada ya kukataa kumpa Khaliyfah mpya wa Waislamu mali ya Zakaah kama walivyokuwa wakimpa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Walisema kuwa Allaah katika aya ya 103 ya Suratu Tawbah anasema;
"Chukua Swadaqah katika mali zao, ziwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (Zakaah) kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu na Allaah ndiye asikiaye na ajuaye."
Waasi hao wakasema:
"Tulitakiwa tutoe Zakaah na kumpa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) apate kututakasa kwa ajili ya hizo Zakaah na kutuombea dua, lakini sasa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kesha kufa na Abu Bakr hawezi kututakasa na kutuombea dua kama alivyokuwa akifanya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa ajili hiyo hakuna tena haja ya kutoa Zakaah."
Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)akaamua kuingia vitani na waasi hao kutokana na sababu mbili;
1- Aliona kuwa huko ni Kurtadi, kwa sababu Zakaah ni nguzo ya tatu ya Kiislamu na kukataa kuitoa ni kuikataa nguzo hiyo.
2- Akaona pia kuwa kuyanyamazia mambo hayo kutasababisha kutokea uasi wa aina nyingine, maana watu watakapoona kuwa pana udhaifu katika uongozi, kila mmoja atataka kuiweka sheria mikononi mwake.
''Umar bin Al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu)yeye aliona kuwa kwa vile watu hao wanaukubali Uislamu, bora wasiwapige vita, lakini Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)aliyekuwa akijulikana kwa upole hakuikubali rai hiyo na akashikilia kupigana na waasi hao.
'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu)akamwambia; "Vipi unapigana vita na watu wanaoikubali shahada ya "Laa ilaaha illa llah" wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kuwa; atakayeikubali shahada hiyo itahifadhika mali yake na damu yake?
Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)akajibu;
"Lakini si alisema kuwa ni lazima aipe haki yake (shahada hiyo)? Na Zakaah ni katika haki zake." 'Umar
Baadhi ya makabila yanayoishi mbali na mji wa Madiynah na ambayo yaliingia karibuni tu katika Uislamu, yalianza kufanya uasi na kurtadi mara baada ya kusikia habari za kifo cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Walirtadi baada ya kukataa kumpa Khaliyfah mpya wa Waislamu mali ya Zakaah kama walivyokuwa wakimpa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Walisema kuwa Allaah katika aya ya 103 ya Suratu Tawbah anasema;
"Chukua Swadaqah katika mali zao, ziwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (Zakaah) kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu na Allaah ndiye asikiaye na ajuaye."
Waasi hao wakasema:
"Tulitakiwa tutoe Zakaah na kumpa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) apate kututakasa kwa ajili ya hizo Zakaah na kutuombea du'aa, lakini sasa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kesha kufa na Abu Bakr hawezi kututakasa na kutuombea du'aa kama alivyokuwa akifanya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kwa ajili hiyo hakuna tena haja ya kutoa Zakaah."
Sayiduna Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu)akaamua kuingia vitani na waasi hao kutokana na sababu mbili;
1- Aliona kuwa huko ni Kurtadi, kwa sababu Zakaah ni nguzo ya tatu ya Kiislamu na kukataa kuitoa ni kuikataa nguzo hiyo.
2- Akaona pia kuwa kuyanyamazia mambo hayo kutasababisha kutokea uasi wa aina nyingine, maana watu watakapoona kuwa pana udhaifu katika uongozi, kila mmoja atataka kuiweka sheria mikononi mwake.
''Umar bin Al-Khatwtwaab (Radhiya Allaahu ‘anhu) yeye aliona kuwa kwa vile watu hao wanaukubali Uislamu, bora wasiwapige vita, lakini Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) aliyekuwa akijulikana kwa upole hakuikubali rai hiyo na akashikilia kupigana na waasi hao.
'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) akamwambia; "Vipi unapigana vita na watu wanaoikubali shahada ya "Laa ilaaha illa llah" wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alisema kuwa; atakayeikubali shahada hiyo itahifadhika mali yake na damu yake?
Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu) akajibu;
"Lakini si alisema kuwa ni lazima aipe haki yake (shahada hiyo)? Na Zakaah ni katika haki zake." 'Umar (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema baadaye kuwaambia watu:
"Kisha Allaah alikifungua kifua changu kuikubali rai ya Abu Bakr".
Alisema baadaye kuwaambia watu:
"Kisha Allaah alikifungua kifua changu kuikubali rai ya Abu Bakr".