21-Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti: Kuacha kuomboleza kwa sauti ni rehema kwa maiti
Kuacha kuomboleza kwa sauti ni rehema kwa maiti:
Tunasoma katika sahihi mbili kuwa, ‘Umar bin Al-Khattab (Radhiya Allaahu 'anhu) alipochomwa kisu, Hafswa, mwanae wa kike akaanza kuomboleza kwa nguvu. Umar akamwambia Hafswa, ‘Ewe Hafswa je hukumsikia Mtume akisema, ‘Mwenye kuliliwa na watu huadhibiwa.’ Na Suhaib akaliliwa vile vile na waliokuwa wanaomboleza namna hiyo wakawa wanalia kwa kusema, ‘Ewe ndugu yangu aa aaah, ewe jamaa yangu aaa aaah, Umar akasema, “Ewe, Suhaib, Je, hujui kuwa mwenye kuliliwa huadhibiwa.’
Katika sahihi mbili, ‘Kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) amesema, “Hakika maiti huadhibiwa kwa kilio cha jamaa zake.”
Katika Riwaya ya Muslim, “Maiti huadhibiwa kaburini kwa kuliliwa na ndugu zake.”
Abdullah bin Rawaha (Radhiya Allaahu 'anhu) alizimia, Amrah dada yake Abdullah akaanza kulia kwa kusema, ‘Wajabalaah, na kadha wa kadha, alipozindukana Abdullah bin Rawaha akasema, ‘ulichokifanya na ulichokisema nimeambiwa, Je, wewe ndivyo ulivyo? Alipofariki Abdullah dada yake hakumlilia tena.’ (Bukhari)