57-Dalili Za Kheri Katika Mambo Yamfaayo Maiti: Kuzuru kaburi lake na kumuombea
Kuzuru kaburi
Ziara ya makaburi ni jambo lililoruhusiwa kisheria, ni jambo lenye faida kwa walio hai ili wawaidhike na iwakumbushe na akhera ajue mwenye kuzuru kaburi kuwa hapo alipo nduguye naye atakuwamo siku moja. Hali kadhalika faida nyingine ni kuwaombea nduguze waislamu na huyo maiti wake. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) amesema, “Nilikuwa nimewakataza kwanza kuzuru makaburi lakini kuanzia sasa yatembeleeni.” (Muslim) katika lafdhi nyingine hadithi inasema, “Kwani huko kuzuru makaburu hukukumbusheni na akhera.” (Ahmad)
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa Sallam) wakati fulani alilitembelea kaburi la mama yake akalia na walio pambizoni mwa Mtume nao wakalia