03-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Huruma/Upole Kwa Mke Wako Unapotaka Kukutana Kinyumba

Inapendekezwa kuwa mtu anapotaka kufanya tendo la ndoa na mkewe katika siku ya kwanza ya ndoa, ambembeleze na amuonyeshe hali ya huruma na upole kama kumkaribisha kinywaji na kadhalika. Kama tunavyojifunza katika Hadiyth ya Asmaa bint Yaziyd ibn As-Sakaan ambaye alisema:

 

إني قَيَّنْتُ عائشة لرسول الله صلى الله عليه وسلّم، ثم جئته، فدعوته لجَلْوَتِهَا، فجاء فجلس إلى جنبها، فُاتي بعُسٍّ لينٍ، فشرب ثم ناوله النبي صلى الله عليه وسلّم فخفضت رأسها واستحيت، قالت أسماء: فانتهرتُها، وقلت لها: خذي من يد رسول الله صلى الله عليه وسلّم، قالت: فأخذت فشربت شيئاً، ثم قال لها النبي صلى الله عليه وسلّم: «أَعْطِي تِرْبَكِ» قالت أسماء: فقلت: يا رسول الله، بل خذه فاشرب منه، ثم ناولنيه من يدك، فأخذه فشرب منه ثم ناولنيه، قالت: فجلست ثم وضعته على ركبتي ثم طفقت أُديره وأُتبعه شَفَتِي لأصيب منه مَشْرَبَ النبي صلى الله عليه وسلّم، ثم قال لنسوة عندي: «نَاوِلِيْهِنَّ» فقلن: لا نشتهيه، فقال النبي صلى الله عليه وسلّم: «لا تَجْمَعْنَ جُوْعاً وكَذِباً»

"Nilimpamba ‘Aaishah kwa ajili ya Mjumbe wa Allaah, kisha nikamwita aje kumfunua na kumuangalia. Alikuja, akakaa pambizoni mwake, akaleta kikombe kikubwa cha maziwa ambayo alikunywa. Kisha akamkaribisha ‘Aaishah ambaye aliinamisha kichwa chake kwa kuona haya. Nikamgombeza na kumwambia: Pokea kutoka kwenye mikono ya Mtume Akachukua na kunywa kidogo. Kisha Mtume akamwambia: ((Wape mengine rafiki zako)) Hapo nilisema: Ee Mjumbe wa Allaah bora chukua mwenyewe na kunywa na kisha unipe mimi kwa mikono yako. Akachukua na kunywa kidogo kisha akanipa mimi. Nikakaa chini na kuyaweka katika magoti yangu. Kisha nikaanza kukizungusha na kukifuatia kwa mdomo wangu ili nifikie pale alipokunywa Mtume. Kisha Mtume akasema kuhusu wanawake waliokuwepo pamoja na mimi: ((Wape wanywe)) Lakini wakasema: Hatuyataki (Yaani hawana njaa). Mtume akasema, ((Msichanganye njaa na uongo))[1]

 

 

 


[1] Ahmad na Al-Humaidiy. Ahmad ameipokea kwa isnaad mbili, kila moja inathibiti nyingine

 

Share