07-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Vipi Mume Akutane Kinyumba Na Mkewe

Mume na mke, wanaruhusiwa kukutana kinyumba, kwa mtindo wowote wanaopenda, lakini tendo la ndoa liwe katika sehemu yake ya mbele tu ya maumbile. Kuhusu hili Allaah Anasema:

 

 

((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَّكُمْ فَأْتُواْ حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ))

 

((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo))  (Al-Baqarah 2: 223) yaani mpendavyo, kwa kupitia nyuma au kupitia mbele

Kuna Hadiyth mbali mbali kuhusu mas-ala haya nitazitaja mbili:

Kwanza:

عن جابر رضي الله عنه قال:  قالتِ اليهودُ: إنَّمَا يكونُ الحَوَلُ إذَا أَتَى الرجُلُ امْرَأَتَهُ من خَلْفِهَا، فأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ((نِسَآؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ)) مِنْ بَيْنِ يَدَيْهَا وَمِنْ خَلْفِهَا وَلاَ يَأْتِيْهَا إِلاَّ في المَأْتَى. 

Imetoka kwa Jaabir رضي الله عنه ambaye amesema Mayahudi walikuwa wakisema kwamba mtoto huwa kengeza ikiwa mwanamume atakutana na mkewe kinyumba kwa mtindo wa nyuma yake. Baada ya hapo Allaah Akateremsha aayah, ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo)) (Al-Baqarah 2: 223)   ((Ikiwa ni kwa mtindo wa kupitia mbele yake au kupitia kwa nyuma yake lakini sehemu ya maumbile ya kukutana iwe ni ya mbele))[1]

Pili:

 

عن ابنِ عَبَّاسٍ، قال: «إنَّ ابنَ عُمَرَ ـ وَالله يَغْفِرُ لَهُ ـ أوْهَماَ إِنَّمَا كَانَ هٰذَا الْحَيُّ مِنَ الأَنْصَارِ وَهُمْ أَهْلُ وَثَنٍ مَعَ هٰذَا الْحَيِّ مِنْ يَهُودَ وَهُمْ أَهْلُ كِتَابٍ وكَانُوا يَرَوْنَ لَهُمْ فَضْلاً عَلَيْهِمْ في الْعِلْمِ، فَكَانُوا يَقْتَدُونَ بِكَثِيرٍ مِنْ فِعْلِهِمْ، وكَانَ مِنْ أَمْرِ أهْلِ الْكِتَابِ أنْ لا يأْتُوا النِّساءَ إلاَّ عَلَى حَرْفٍ، وَذٰلِكَ أسْتَرُ ما تَكُونُ المَرْأةُ، فَكَانَ هٰذَا الْحَيُّ مِنَ الأَنْصَارِ قَدْ أخَذُوا بِذٰلِكَ مِنْ فِعْلِهِمْ، وَكَانَ هٰذَا الْحَيُّ مِنْ قُرَيْشٍ يَشْرَحُونَ النِّسَاءَ شَرْحاً مُنْكَراً، وَيَتَلَذِّذُونَ مِنْهُنَّ مُقْبِلاَتٍ ومُدْبِرَاتٍ وَمُسْتَلْقِيَاتٍ، فَلَمَّا قَدِمَ المُهَاجِرُونَ المَدِينَةَ تَزَوَّجَ رَجُلٌ مِنْهُمْ امْرَأَةً مِنَ الأَنْصَارِ، فَذَهَبَ يَصْنَعُ بِهَا ذٰلِكَ فَأَنْكَرَتْهُ عَلَيْهِ وَقَالَتْ إِنَّمَا كُنَّا نُؤْتَى عَلَى حَرْفٍ فَاصْنَعْ ذٰلِكَ، وَإِلاَّ فَاجْتَنِبْنِي حَتَّى شَرِيَ أَمْرُهُما، فَبَلَغَ ذٰلِكَ رَسُولَ الله صلى الله عليه وسلم فَأَنْزَلَ الله عَزَّوَجَلَّ:  ((نِسَاؤُكُمْ حَرْثٌ لَكُمْ فَأْتُوا حَرْثَكُمْ أَنَّى شِئْتُمْ)) أيْ مُقْبِلاَتٍ وَمُدْبِرَاتٍ وَمُسْتَلْقِيَاتٍ يَعْنِي بِذٰلِكَ مَوْضِعَ الْوَلَدِ
 

Imetoka kwa Ibn 'Abbaas رضي الله عنهما ambaye amesema: "Kwamba Ibn 'Umar na Allaah Amghufurie au Awaghufurie. Maanswari ambao walikuwa wapagani wakiabudu miungu mingi. Waliishi na Mayahudi ambao ni Ahlul-Kitaab. Maanswari wakaona kwamba Mayahudi ni bora kuliko wao katika elimu na walikuwa wakifuata mifano yao katika mambo mengi. Watu wa vitabu walikuwa wakifanya mapenzi (kujimai) na wake zao kwa (kuwaingilia upande) hii ikiwa ni njia ya staha kabisa kwa mwanamke na Maanswari wakafuata mfano wao huo. Watu hawa kutoka Quraysh, upande mwingine walikuwa wakiwafichua wanawake wao katika njia isiyopendeza. Wakistarehe nao kwa mitindo ya kupitia mbele (mtindo wa kuelekeana uso kwa uso), kupitia kwa nyuma (au mtindo wa kuwainamisha), au wakiwalaza chali. Muhaajiruun walipohamia Madiynah, mmoja wao alimuoa mwanamke kutoka kwa Answaar. Akaanza kumfanyia hivyo (mitindo hiyo) lakini (mwanamke) akamkatalia na kumwambia: Sisi tulikuwa tunakutana kinyumba kutoka upande, kwa hiyo fanya hivyo au jitenge nami!" Mabishano yao yakamfikia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kisha Allaah سبحانه وتعالى Akateremesha Aayah ((Wake zenu ni kama konde zenu. Basi ziendeeni konde zenu mpendavyo)) Yaani kupitia mbele au nyuma, au kulazwa chali. Iliyokusudiwa ni sehemu inayotoa watoto.”[2]

 

 

 

[1] Al-Bukhaariy na Muslim

[2] Abu Daawuud, Al-Haakim na wengineo ikiwa isnaad yake ni hasan

 

Share