15-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kukoga Ni Bora Kabla Ya Kulala

 

 

Inapendeza kukoga kuliko uwezekano uliotajwa hapo juu (wa kutawadha baada ya janaba kabla ya kulala) kama ilivyo wazi katika Hadiyth ya 'Abdullah ibn Qays ambaye amesema,

 

سَأَلْتُ عَائِشَةَ كَيْفَ كَانَ كان صلى الله عليه وسلم  يَصْنَعُ فِي الْجَنَابَةِ؟ أَكَانَ يَغْتَسِلُ قَبْلَ أَنْ يَنَامَ أَمْ يَنَامُ قَبْلَ أَنْ يَغْتَسِلَ؟ قَالَتْ: كُلُّ ذٰلِكَ قَدْ كَانَ يَفْعَلُ، رُبَّمَا اغْتَسَلَ فَنَامَ، وَرُبَّمَا تَوَضَّأَ فَنَامَ. قُلْتُ: الْحَمْدُ لله الَّذِي جَعَلَ فِي الأَمْرِ سَعَةً

 

"Nilimuuliza mama wa waumini ‘Aaishah vipi Mtume alikuwa akifanya katika hali ya janaba? Je, alikoga kabla ya kulala au alilala kabla ya kukoga?" Alijibu: "Alifanya vyote hivyo, mara nyingine alikoga kisha akalala na mara nyingine alitawadha kisha akalala". "Nikasema: Sifa zote Anastahiki Allaah Aliyejaalia wepesi mkubwa katika jambo hili".[1]

 

 

 

 



[1] Muslim, Ahmad na Abu 'Awwaanah

Share