25-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Makatazo Ya Kutangaza Siri Za Chumbani

Inakatazwa aidha mume au mke kueneza siri zao zozote za chumbani kwa mtu yeyote wa nje. Hadiyth zifuatazo zimekataza hivyo:

 

Kwanza:

 

((إِنَّ مِنْ أَشَرِّ النَّاسِ عِنْدَ اللّهِ مَنْزِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ، الرَّجُلَ يُفْضِي إِلَى امْرَأَتِهِ، وَتُفْضِي إِلَيْهِ، ثُمَّ يَنْشُرُ سِرَّهَا))

((Hakika miongoni mwa watu waovu kabisa siku ya Qiyaamah ni mwanamume anayemuingilia mkewe kwa jimai akamuitikia, kisha akaeneza siri zake))[1]

 

Pili:

 

عن أسماء بنت يزيد : أنها كانت عند رسول الله صلى الله عليه وسلّم ، والرجال والنساء قعود عنده . فقال: ((لَعَلَّ رَجُلاً يَقُولُ ما يَفْعَلُ اهْلِهِ، وَلَعَلَّ امْرَأَةً تُخْبِرُ بِمَا فَعَلَتْ مَعَ زَوْجِهَا؟)) ازَمَّ القَوْمُ، فَقلت: أي والله يا رسول الله، إنهم ليفعلون، وإنهنّ ليفعلن، قال: ((فَلا تَفْعَلُوا، فًّانَّمَا مَثَلُ ذَلِكَ مَثَلُ شَيْطانٍ لَقِيَ شَيْطَانَةً فَغَشِيَهَا وَالنَّاسُ يَنْظُرُونَ))

 

Imetoka kwa Asmaa bint Yaziyd ambaye amesema: "Alikuwa kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  na walikuweko wanaume na wanawake wamekaa. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Huenda mume akajadiliana anayoyafanya na mkewe au huenda mwanamke akamhadithia mtu aliyoyafanya na mumewe?)) Watu walikuwa kimya. Kisha nikasema: 'Ee Mjumbe wa Allaah, hakika wanaume na wanawake wote hunafanya hivyo'. Kisha Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Msifanye hivyo kwani ni kama mfano shaytwaan mwanamume amekutana na shaytwaan mwanamke njiani wakawa wanafanya jimai na huku watu wanawatazama))[2]

 

 

[1] Muslim, Ibn Abi Shaybah, Ahmad na wengineo

[2] Ahmad: Hasan au Swahiyh kutokana na kukubaliana (na masimulizi mengine)

Share