37-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Kuwaombea Bwana Harusi Na Bibi Harusi Watoto Wengi (Wa Kiume) Ni Msemo Katika Ada Ya Ujahiliya (Kabla Ya Uislam)
Haipasi kusema "Ujaaliwe watoto wengi wa kiume"
عَنِ الْحَسَنِ قَالَ: تَزَوَّجَ عَقِيلُ بْنُ أَبِي طَالِبٍ امْرَأَةً مِنْ بَنِي جَثمٍ فدخل عليه القوم، فقالوا "بِالرِّفَاءِ وَالْبَنِينِ" فقَالَ: لا تفعلوا ذلك [فإن رسول الله صلى الله عليه وسلم نهى عن ذلك]، قَالُوا فَمَا نَقُول يآ أبا زَيْد؟ قَال: قُولُوا( كَمَا قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم): ((بَارَكَ اللَّهُ فِيكُمْ وَبَارَكَ لَكُمْ)). ( إنا كذلك كنا نؤمر)
Imetoka kwa Al-Hasan رضي الله عنه kwamba 'Uqayl ibn Abi Twaalib alimuoa mwanamke kutoka kabila la Jathm. Watu walikuja nyumbani kwake na wakasema: "Ujaaliwe kupata watoto wengi wa kiume". 'Uqayl akawaambia: 'Msifanye hivyo, kwani Mtumeصلى الله عليه وآله وسلم amekataza hivyo'. Wakasema: Sasa tuseme nini ewe Abu Zayd? Akasema: Semeni kama alivyosema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ((Allaah Akubariki na Ateremshe Baraka juu yenu)). (Hivyo ndivyo tulivyoamrishwa kusema)"[1]