42-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Nasaha Kwa Mume Na Mke

 

Kwa kumalizia, natoa Nasaha zifuatazo kwa mume na mke

 
Kwanza:

-  Wanasihiane katika kumtii Allaah

 
- Wafuate amri za Allaah zilizomo kwenye Qur-aan na Sunnah

- Wasitangulize desturi na mila zao au madhehebu yao juu ya hukumu za kisheria alizoweka Allaah

Allaah Anasema:

((وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا))

 

"Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Allaah na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Allaah na Mtume Wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi" (Al-Ahzaab: 36)

 

Pili:

 

Kila mmoja wao atimize mas-uliyya yake aliyowajibishwa na Allaah سبحانه وتعالى Amemuwajibishia. Kwa hiyo mke asidai haki sawa na za mume katika haki zake zote na mume asitumie cheo chake alichofadhilishiwa na Allaah cha uongozi na mamlaka kwa kumkandamiza na kumdhulumu mke, kumpiga au kumuonea bila ya haki yoyote ile.

 

Allaah سبحانه وتعالى Anasema:

 

((وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ وَاللّهُ عَزِيزٌ حَكُيمٌ))

  

((Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Allaah ni Mwenye Nguvu na Mwenye Hikima)) [Al-Baqarah: 228]

 

Katika Aayah nyingine Allaah سبحانه وتعالى Anasema:

 

((الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاء بِمَا فَضَّلَ اللّهُ بَعْضَهُمْ عَلَى بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُواْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللّهُ وَاللاَّتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَاهْجُرُوهُنَّ فِي الْمَضَاجِعِ وَاضْرِبُوهُنَّ فَإِنْ أَطَعْنَكُمْ فَلاَ تَبْغُواْ عَلَيْهِنَّ سَبِيلاً إِنَّ اللّهَ كَانَ عَلِيًّا كَبِيرًا))

 

((Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Allaah baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayoitoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika utiifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikutiini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Allaah Ndiye Aliye juu na Mkuu)) [An-Nisaa: 34]

 

 

  وقد قال مُعَاوِيَةَ بن حيدة رضي الله عنه: يَارَسُولَ الله مَا حَقُّ زَوْجَةِ أَحَدِنَا عَلَيْهِ؟ قال: ((أَنْ تُطْعِمَهَا إذَا طَعِمْتَ، وَتَكْسُوَهَا إذَا اكْتَسَيْتَ وَلا تُقَبِّحْ وَلاتَضْرِبِ الْوَجْهَ، ( وَلا تَهْجُرْ إلاَّ في الْبَيْتِ كَيْفَ وَقَدْ أَفْضَى بَعْضكُمْ إِلَى بَعْضٍ؛ إِلاَّ بِمَا حلَّ عَلَيْهِنَّ)

 

 

وقال صلى الله عليه وسلم : ((الْمُقْسِطُونَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَى مَنَابِرَ مِنْ نُورٍ عَنْ يَمِينِ الرَّحْمٰنِ وَكِلْتَا يَدَيْهِ يَمِينٌ، الْمُقْسِطُونَ عَلَى أَهْلِيهِمْ وَأَوْلاَدِهِمْ وَمَا وَلُّوا))

 

Mu'aawiyyah bin Haydah رضي الله عنه amesema: "Ewe Mjumbe wa Allaah, haki gani wake zetu wanazo juu yetu?" Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Muwalishe kama mnavyojilisha wenyewe, muwavishe kama mnavyojivisha wenyewe, wala msiwaombee ubaya, (hii ni kutokana na mila ya Waarabu kabla ya Uislamu wakiwaombea wake zao wanapokuwa na ghadhabu, "Allaah akujaalieni sura mbaya", msiwapige usoni mwao, na katika kuhama malezi msitoke nje ya nyumba kulala. Vipi (mtafanya mambo hayo) na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, kwa hiyo fanyeni yale yaliyoruhusiwa kuwafanyia)) (iwe kwa sababu inayokubalika na shariy'ah"[1]   (katika riwaaya nyingine) Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  amesema, ((Wafanyao uadilifu watakuwa katika minbar ya mwangaza upande wa kulia wa Allaah na Mikono yote ya Allaah ni ya kulia[2], wale waliokuwa na uadilifu katika familia zao na kwa yote waliyopewa mamlaka))[3]

 

Wote wawili watakapojua na kutekeleza haya, Allaah سبحانه وتعالى Atawajaalia maisha mema na wataendelea kuishi hivyo hivyo maadamu watakuwa pamoja katika furaha na raha mustarehe. 

 

Anasema Allaah سبحانه وتعالى:

 

((مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ))

 
((Wafanyaji mema, wanaume au wanawake, hali ya kuwa ni Muumini, Tutawahuisha maisha mema; na Tutawapa ujira wao mkubwa kabisa kwa sababu ya yale mema waliyokuwa wakiyatenda)) (An-Nahl: 97)

 
 

Tatu:

Mwanamke khaswa inampasa kuwa mtiifu kwa mumewe kwa kadiri ya uwezo wake. Na hii ndivyo Allaah Alivyowafadhilisha wanaume juu ya wanawake kama ilivyo katika aayah mbili zifuatazo:

 

ِ((وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ))

  

((Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao)) (Al-Baqarah: 228

 

((الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاء))

 

 ((Wanaume ni wasimamizi wa wanawake)) (An-Nisaa: 34)

Kuna Hadiyth nyingi Swahiyh ambazo zimesisitiza maana hii, nazo zimeelezea dhahiri haki za mwanamke akiwa ni mtiifu au sio mtiifu. Ni muhimu kuzitaja baadhi ya Hadiyth hizo kama ni ukumbusho kwa wanawake wetu wa siku hizi kwa vile Allaah سبحانه وتعالى Anasema:

 

 

 

 ((وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَى تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ))

 

((Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini)) (Ad-Dhaariyaat: 55)

 

 
Kwanza:

 

((لا يَحِلُّ للمرأةِ ان تصومَ ( وفي رواية) (لاَ تَصُمِ الْمَرْأَةُ) وَزَوْجُهَا شَاهِدٌ إلاَّ بِإذْنِهِ (غَيْرِ شَهْرِ رَمَضَانَ) ولا تأذَن في بيته إلا بإِذنِهِ))

 

((Haimpasi mwanamke kufunga na wakati mumewe yupo ila kwa ruhusa yake isipokuwa Ramadhaan na wala asimruhusu mtu yeyote kuingia nyumbani kwake ila kwa ruhusa yake))[4]

 

Pili:

 

((إِذَا دَعَا الرَّجُلُ امْرَأَتَهُ إِلَى فِرَاشِهِ، فَلَمْ تَأْتِهِ، فَبَاتَ غَضْبَانَ عَلَيْهَا، لَعَنَتْهَا الْمَلاَئِكَةُ حَتَّى تُصْبِحَ)) وفي رواية: ((أَوْحَتَّى ترجع))، وفي أخرى: ((حَتَّى يُرْضى عَنْهَا))

 

((Mume atakapomwita mkewe kitandani na akikataa mke, na mume akawa ameghadhibika, basi Malaika watakuwa wanamlaani huyo mke mpaka asubuhi)) (katika riwaaya nyingine) ((Mpaka arudi kwake)) (na riwaaya nyingine) ((Mpaka aridhike naye))[5]

 

Tatu:

 

((وَالَّذِي نَفْسُ مُحَمَّدٍ بِيَدِهِ لاَ تُؤَدِّي الْمَرْأَةُ حَقَّ رَبِّهَا حَتَّى تُؤَدِّيَ حَقَّ زَوْجِهَا وَلَوْ سَأَلَهَا نَفْسَهَا، وَهِيَ عَلَى قَتَبٍ، لَمْ تَمْنَعْهُ))

 

((Naapa kwa Yule Ambaye Nafsi ya Muhammad imo Mikononi Mwake, mwanamke atakuwa hakutimiza haki ya Mola wake hadi atimize haki ya mumewe, hata kama akimtaka akiwa juu ya tandiko la farasi, (basi hatakiwi) kumkatalia ombi lake))[6]

 

Nne:

 

((لاَ تُؤْذِي امْرَأَةٌ زَوْجَهَا فِي الدُّنْيَا  إِلاَّ قَالَتْ زَوْجَتُهُ مِنَ الْحُورِ الْعِينِ: لاَ تُؤْذِيهِ. قَاتَلَكِ اللَّهُ فَإِنَّمَا هُوَ عِنْدَكِ دَخِيلٌ أَوْشَكَ أَنْ يُفَارِقَكِ إِلَيْنَا))

 

((Kila mara mke anapomuudhi mumewe duniani, mke wake katika Mahuurul-'Ayn (Wake wa Peponi) husema: Usimuudhi, Allaah Akuangamize! Kwani yeye kwako ni mgeni tu, na karibu ataachana na wewe atatujia sisi))[7]

Tano:

 

عن حُصَيْنٍ بنِ مِـحْصَنٍ قالَ حدثتنـي عَمَّتِـي قالتْ: أتـيتُ رسولَ الله فـي بعضِ الـحاجةِ قالَ: «إِيْ هذِهِ أَذَاتُ بَعْلٍ أَنْتِ»، قلتُ: نَعَمْ، قال: «فكيفَ أَنْتِ لَهُ»، قالتْ: (فَقُلْتُ:) ما آلوهُ إلاَّ مَا عَجَزْتُ عنهُ، قالَ: «فأَيْنَ أَنْتِ منهُ، فإنَّـمَا هو جَنَّتُكِ ونَارُكِ»

 

Kutoka kwa Huswayn bin Mihswan ambaye amesema: "Shangazi yangu alinisimulia (Hadiyth) akisema, 'Nilikwenda kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم nikiwa nimehitaji baadhi ya haja, akasema, ((Ewe fulani! Je, umeolewa?)) Nikasema, "Ndio". Akaniuliza, ((Uko vipi na mumeo?)) Nikajibu, "Sina upungufu wowote kwake isipokuwa yale nisiyoyaweza kufanya". Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema, ((Basi jiangalie hali yako katika uhusiano wako kwake, kwani yeye ni ufunguo wako wa Pepo na Moto))[8]

 
Sita:

((إذا صَلَّتِ المَرْأَةُ خَمْسَها، (وصَامَتْ شَهْرَها)، وحَصَّنَتْ فَرْجَهَا، وأطَاعَتْ بَعْلَهَا، دَخَلَتْ مِنْ أيِّ أبوابِ الجَنَّةِ شَاءَتْ))

 

((Mwanamke atakaposwali Swalah zake tano, akahifadhi sehemu zake za siri (asifanye uzinifu), akamtii mume wake, ataingia peponi kupitia mlango wowote autakao))[9]

 

 


[1] Ahmad: Swahiyh

[2] Allaah ana mikono miwili na mikono yote miwili ni ya kulia. Uzindushi: Ahlu Sunnah wal Jama’ah wote humsifu Allaah kama Alivyojisifu mwenyewe au kama alivyosifiwa na Mtume Wake bila ya kuzidisha au kupunguza au kubadilisha jina au sifa yoyote ile, na wakati huo huo hawamfananishi Allaah na chochote kati ya alivyoviumba (Rejea Surat Shuuraa ayah ya 11)

Nu’aym bin Hammaad Shaykh wa Imaam Al-Bukhaariy amesema, ‘Mwenye kumfananisha Allaah na viumbe Vyake amekufuru. Na anayezikanusha sifa alizojisifia nazo Allaah Mwenyewe kwa kuisifia Nafsi Yake amekufuru. Na hakuna katika sifa alizojisifia nazo Allaah wala kusifiwa na Mtume Wake upinzani (Mfasiri)

[3] Muslim

[4] Al-Bukhaariy na wengineo

[5] Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo

[6] Ibn Maajah, Ahmad na wengineo: Swahiyh

[7] At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na wengineo: Swahiyh

[8] At-Twabaraaniy katika 'Al-Awrat', Ibn Maajah na Ahmad: Swahiyh

[9] At-Twabaraaniy katika 'Al-Awrat', Ibn Hibbaan na wengineo: Hasan au Swahiyh

 

 

Share