Ufafanuzi Wa Swali La Zakaah Ikiwa Mtaji Unaongezeka
SWALI
Asalaam aleikum,
Alhamdulilah, kwa kulijibu suala langu la zaka lakini bado sijaridhika. Kipengele cha pili ndilo suala langu, yaani kutimia mwaka. Katika hizo 1500, bado nyengine zitakua hazijatimia mwaka na mara nyengine tafauti hua kubwa kwa mamilion kiasi ya mwezi tu kufikia mwezi wa kutoa zaka. Nielezeni nisijidhulumu wala nisidhulumu.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako
Swali la mwanzo, jibu lake linapatikana katika kiungo kifuatacho:
Zakaah Ikiwa Mtaji Unaongezeka Itolewa Vipi?
Jibu kwa suala lililo juu yaonyesha limeleta utata kwa muulizaji, ambaye amelirudisha tena katika ukumbi. Mara nyingi wengi wetu hutumia mantiki katika mas-ala ya Kidini na mara nyingine mantiki na akili hii huwa haifanyi kazi na matokeo yake huleta natija mbaya. Kwa ajili hiyo ndiyo ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya Allaahu ‘anhu) akasema: “Ikiwa Dini inakwenda kwa rai (mantiki) basi ingekuwa kupangusa khufu (soksi za ngozi [wakati wa wudhuu]) ni chini (kwenye uchafu) na siyo juu yake, lakini hivi ndivyo nilivyomuona Mtume akifanya [akipangusa juu na si chini]”.
Tukirudi katika suala lako ni kuwa mwanzo hakuna mtu katika dunia hii ambaye pesa zake zinaongezeka kwa mamilioni
Hakika ni kuwa Zakaah ni usaidizi kwa masikini, faradhi kwa matajiri, thawabu nyingi na ni nyongeza/ ziada kwa mtoaji. Kwa hivyo mtoaji
Na Allaah Anajua zaidi