11-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Hukmu Ya Asiyelipa Zakaatul-Fitwr Japokuwa Ana Uwezo

Hukmu Ya Asiyelipa Zakaatul-Fitwr Japokuwa Ana Uwezo

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Nini hukmu ya mwenye uwezo wa kutoa Zakaatul-Fitwr lakini hatoi?

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah,

 

Asiyetoa Zakaatul-Fitwr lazima afanye Tawbah kwa Allaah na aombe maghfirah kwa sababu anapata dhambi kuizuia. Itambidi pia ailipe kwa wanaostahiki kuipokea, lakini ikiwa baada ya Swalaah ya 'Iyd itahesabika kama ni sadaka ya kawaida.

 

 

 

Wa biLLaahi at-tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]

 

 

Share