15-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Zakaatul-Fitwr Kwa Ajili Ya Mtoto Aliye Tumboni
Zakaatul-Fitwr Kwa Ajili Ya Mtoto Aliye Tumboni
Al-Lajnah Ad-Daaimah
SWALI:
Zakaatul-Fitwr ilipwe kwa ajili ya mtoto aliye bado tumboni mwa mama?
JIBU:
Inapendekezeka kulipa kwa sababu 'Uthmaan (Radhiya Allaahu 'anhu) alifanya. Lakini sio fardhi bali ni jambo linalopendezeka tu.
Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah]