20-Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kamlipia Zakaatul-Fitwr Mtoto Aliye Tumboni Akaja Kujua Kwamba Ni Mapacha

Kamlipia Zakaatul-Fitwr Mtoto Aliye Tumboni Akaja Kujua Kwamba Ni Mapacha

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Mke wangu alikuwa mja mzito mwezi wa Ramadhwaan, nikalipa Zakaatul-Fitwr kwa ajili ya mtoto aliye tumboni. Alipokuja kujifungua siku chache baada ya 'Iyd kumbe walikuwa ni mapacha kwa uwezo wa Allaah. Je, napaswa kufanya nini sasa na hali nilitoa Zakaatul-Fitwr kwa ajili ya mtoto mmoja aliye tumboni na sio wa pili?

 

JIBU:

 

 

Huna haja ya kufanya lolote kwa kutokumlipia mtoto wa pili Zakaatul-Fitwr.

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyina Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.

 

[Fataawaa Al-Lajnah Ad-Daaimah (9/366)]

 

 

 

Share